Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 January 2015
Thursday, January 22, 2015

Real Madrid yasajili kinda.


Na Chikoti Cico

Klabu ya Real Madrid kutoka nchini Hispania imekubali kumsajili kinda wa miaka 16 kutoka klabu ya Stromsgodset ya nchini Norway Martin Odegaard ambaye amekuwa akiwaniwa na klabu mbalimbali barani Ulaya.

Madrid ambao hawajaweka wazi ada ya mchezaji huyo wala mshahara wake lakini taarifa kutoka vyombo vya habari nchini Hispania zinasema Madrid wamekubali kulipa ada yenye karibu kufikia pauni milioni 230,0000 huku kinda huyo akitegemewa kuchukua mshahara wa pauni 80,000 kwa wiki.

Taarifa kutoka kwenye mtandao wa Real Madrid zinasema Odegaard ambaye pia alitaka kusajiliwa na klabu za Manchester United, Liverpool, Barcelona na Bayern Munich anatarajiwa kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari siku ya Alhamisi (leo).

Mchezaji huyo alivunja rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kabisa kucheza mchezo wa kimataifa kwa timu ya taifa ya Norway baada ya kuanza kwenye mechi dhidi ya Falme za Kiarabu uliochezwa mwezi Agasti mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 15 na siku 253.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!