Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 January 2017
Tuesday, January 31, 2017

BIABIANY AIPIGA CHINI CHELSEA









Na FLORENCE GR

Kwa mujibu wa sky sport nchini italia inaripotiwa kuwa winga wa klabu ya soka ya Inter Milan Jonathan Biabiany amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya soka ya Chelsea ambao ni vinara wa ligi kuu Uingereza kwa sasa wakiwa na pointi 55.

Mfaransa huyo amekuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Inter msimu huu ambapo amefanikiwa kucheza mechi tatu tu katika mashindano yote aliyoichezea Inter.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye amechezea timu mbalimbali kama vile Chievo, Parma na Sampdoria amekataa kujiunga kwa mkopo na kutaka kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho hata kama hatapata namba kunako kikosi cha kwanza.

Biabiany ambaye mwaka 2015 alihusishwa kijiunga na klabu ya Liverpool mara baada ya timu yake ya zamani Parma kufilisika.

Chelsea wamekuwa wakifanya juhudi mbalimbali ya kuimarisha kikosi chao mara baada ya kuondokewa na wachezaji Oscar ambaye ametimkia ligi ya china huku Obi Mikel pia akiondoka klabuni hapo huku wakiwa na hati hati ya kuwapoteza  Branislav Ivanovic na Asmir Begovic ambao wanataka kuondoka klabuni hapo.

Chelsea wanahusishwa juu ya kumuhitaji mshambuliaji wa Swansea city  Fernando Llorente ,mshambuliaji wa Celtic  Moussa Dembele pamoja na Craig Gordon ambaye ni kipa wa Celtic.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!