Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 March 2014
Tuesday, March 25, 2014

BEKI WA BAYERN MUNICH AONGEZA MKATABA.

Difenda wa kati wa Bayern Munich Dante ameongeza mkataba wake katika klabu hiyo iliyoshinda mataji matatu msimu uliopita, na sasa atakaa huko hadi 2017, klabu hiyo ilisema Jumatatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, aliyejiunga nao kutoka Borussia Moenchengladbach mwaka 2012, alijivunia ufanisi mkubwa msimu wake wa kwanza kwa kushinda Bundesliga na German Cup na pia Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. 


"Dante amekuwa bila shaka mmoja wa wachezaji wazuri zaidi tulionunua miaka ya hivi majuzi,” alisema afisa mkuu mtendaji Karl-Heinz Rummenigge kupitia taarifa. "Amekua na kuwa mmoja wa wachezaji wetu muhimu zaidi uwanjani nan je ya uwanja.”

Mchezaji huyo wa miaka 30 aliitwa mara ya kwanza kuchezea Brazil mwaka jana na anatumai kwamba atapata fursa ya kucheza Kombe la Dunia litakalochezewa kwao Juni.
Bayern, ambao watakutana na Manchester United katika robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi ujao, watatwaa taji la Bundesliga leo Jumanne kama watashinda Hertha Berlin.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!