GHANA USO KWA USO NA DR CONGO
Na FLORENCE GR
Michuano ya kombe la matifa ya Africa AFCON yanatarajiwa kuendelea kutimbua vumbi leo katika nchi ya Gaboni kwa robo fainali mbili kuchezwa.
Mabingwa mara nne wa michuano timu ya Ghana 'Black stars' watakuwa na kazi pevu pale watakapovaana na vijana wa DR Congo ambao wamemaliza wakiwa wa kwanza kwenye kundi lao lilokuwa na timu kama Togo na mabingwa watetezi waliotolewa kwenye michuano hiyo timu ya Ivory Cost.
Ghana ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa Chelsea Avram Grant walianza michuano hiyo kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Uganda huku wakionekana kutoonyesha kiwango kikubwa kama ilivyokuwa ikitarajiwa .
Ghana walijihakikishia kucheza robo fainali baada ya kuifunga Mali goli 1-0 kabla ya kufungwa goli 1-0 kutoka kwa mafarao wa Misri mechi ambayo hawakuwa na presha kwani tayari walikuwa wameshafuzu tayari.
Kwa upande wa kikosi cha DR Congo kocha Florent Ibenge ameonekana kuijenga timu hiyo kuwa ngumu kufungika na wamefanikiwa kudhihirisha hiyo baada ya kuifunga timu ya Morocco goli 1-0 na kutoa sare dhidi ya mabingwa watetezi Ivory cost ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa kutetea ubingwa huo.
NJIA KUELEKEA ROBO FAINALI
DR Congo wamefanikiwa kufuzu robo fainali wakiwa wiongozi wa kundi C maraa baada ya kuibuka na ushindi katika michezo miwili na kutoa sare mechi moja
DR Congo 1- Morocco 0
Ivory cost 2- DR Congo 2
DR Congo 3- Togo 1
Kwa upande wa Ghana wenyewe wamemaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Misri baada ya kushinda michezo miwili na kufungwa mmoja
Ghana 1- uganda 0
Ghana 1- Mali 0
Misi 1- Ghana 0
Ghana bado hawana uhakika kama nahodha wao Asamoah Gyan atacheza mchezo huo au laaa!!!! mara baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Misri huku Mubarak Wakaso, Thomas Partey, Jordan Ayew na Frank Acheampong wakitegemewa kurudi kikosini mara baada ya kupumzisha kwenye mchezo dhidi ya Misri.
Kwa upande wa DR Congo wenyewe hawana majeruhi ya mchezaji yoyote yule na wako tayari kuivaa timu hiyo ambayo ilishindwa kuchukua ubingwa huo AFCON iliyopita nchini Equatorial Guinea mara baada ya kufungwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati 8-7 dhidi ya Ivory Cost.
WACHEZAJI WA KUWAANGALIA
Junior Kabananga (DR Congo)
Mchezaji huyo anayekipiga katika klabu ya Astana nchini Kazakhstan ndiye anaeongoza kwa upachikaji wa mabao katika michuano hiyo magoli matatu huku akiwa maefunga katika kila mechi za makundi walizocheza hivyo Ghana wanakazi ya kumchunga kuhakikisha haleti madhara golini kwao huku kocha Ibenge anaamini kuwa nyota huyo atawasaidia kuingia nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 walipofanya hivyo nchini Burkina Faso.
Christian Atsu (Ghana)
Nyota huyo anaekipiga katika klabu ya Newcastle united ya nchini Uingereza amekuwa na mchango mkubwa katika mechi walizocheza huku akisumbua beki za timu pinzani hivyo ataongoza jahazi lla Ghana kufanikiwa kutwaa taji hili ambalo hajatwaa tangu mwaka 1982.
0 comments:
Post a Comment