Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 July 2013
Saturday, July 13, 2013

christiano ronaldo kwenda monaco

Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo imeripitiwa kwamba alikutana na Bilionea wa ki-Russia anayemiliki klabu ya Monaco
wiki iliyopita kuzungumzia uwezekano wa uhamisho dirisha la usajili lijalo.

M-Portuguese huyo amekua akihusishwa na uvumi wa kuihama Real tokea mwaka jana na hasa dirisha hili la usajili baada ya mikutano tabribani mitatu kati ya wawakilishi wake na wale wa Real madrid kushindwa kuafikiana na kuahirishwa mara kwa mara kwa mazungumzo mengine.

Pia Manchester United na Paris Saint-Germain inaaminika wanamtamani, ripoti kutoka France sasa zimeiongeza klabu ya Monaco katika mbio hizo.

Akiwa katika likizo na promosheni zake za kimatangazo wiki iliyopita, inaaminika kwamba staa huyo mwenye miaka 28 alikutana na mmiliki wa MOnaco, Dmitry Rybolovlev.

Bilionea inaripotiwa alichukua fursa hiyo, limeandika gazeti la Le10Sport kujaribu kumshawishi Ronaldo kusaini katika klabu yake majira ya joto yajayo, kama, hatoongeza mkataba wake wa sasa na Los Blancos, kama hatofanya hivyo basi atakua amebakiza mwaka 1 - muda ambao kisheria anaruhusiwa kuongea na klabu yoyote bila ruhusa ya klabu yake ya wakati huo.

Inafahamika kwamba ajenti wa Ronaldo, Jorge Mendes, pia alikuwepo katika mkutano huo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!