Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 April 2015
Friday, April 17, 2015

Pep Guardiola athibitisha msemo wa tenda wema siku zote, usingoje shukrani



  • Na George Mganga, Dar es salaam +255688665508
    Tunapozungumzia makocha wenye hadhi na umaarufu mkubwa hapa duniani siku zote unapotaja orodha ya makocha hao hautoweza kuliacha jina la Pep Guardiola likiwa katika orodha hiyo kwani utakuwa umekosea sana sababu ni mtu ambaye amekuwa na mafanikio makubwa mno akiwa kama Mwalimu wa soka katika wadhifa "Career" yake katika maisha yake kufikia hapa alipo sasa.
    Sitopenda kuizungumzia historia yake kwa kirefu kwa kirefu ila kuna machache ambayo nimeyaandaa kukujuza wewe kile ambacho hukifahamu na inawzekana kabisa unakijua lakini sio vibaya tukikumbushana na hii ni asili ya binadamu kuwa hakuna linalokumbukwa kichwani haswa mtu anapofunzwa bila kurudia kwenye dokuments au majarida ili kupata fursa ya kukumbuka zaidi.
    Pep Guardiola wakati akiwa Mwalimu wa Fc. Barcelona ameweza kuitumikia timu hiyo na ndani ya miaka mitatu alifanikiwa kuwa na mataji kumi na tatu (13) kimbindoni jambo ambalo sio rahisi kwa kila kocha kulifanya na inahitaji moyo wa uvumilivu sana kulifanya na kufikisha hizo ndoto za kutwaa mataji hayo katika kazi hii ya mpira wa miguu kama Mwalimu.
    Pep amefanikiwa kutwaa mataji mbalimbali akiwa na kilabu ya Barcelona ikiwemo Ligi Kuu nchini humo Hispania, Kombe la Mfalme, Kombe la dunia kwa ngazi ya vilabu alipoifunga Santos ya Brazil halikadhalika pia aliweka rekodi katika career yake ya kutwaa mataji sita (6) mfululizo ndani ya mwaka mmoja ikiwepo kombe la UEFA msimu ambao aliifunga Manchester United na kumtetemesha Sir Alex Fergusson katika dimba la Wembley Stadium kwa ushindi mnono wa goli 3-1 huku United wakiwa katika kiwango bora kabisa.
    Pep katika upande upande wa pili sasa mara baada ya kuondoka Fc. Barcelona alitimkia katika nchi nyingine Ujerumani ili kuendeleza kazi yake na alijiunga na kilabu ya Bayern Munich, kilabu ambayo ameweza kupata sifa lukuki na kuzidi kujiweka katika historia nzuri zaidi kwa kuzidi kujinyakulia mataji mengi zaidi ambapo hadi sasa ameshatwaa taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya na halikadhalika ameshatwaa taji la ligi kuu nchini humo jambo ambalo sio rahisi kwa kila mwalimu kufanya hivyo.
    Tunachokiona hivi sasa katika kilabu ya Bayern Munich hali imeanza kuwa na sintofahamu na hii ni kama "timbwili" ambalo limeanzia usiku wa ulaya siku ya Jumatano mara baada ya timu hiyo kufungwa goli 3-1 dhidi ya Fc. Porto ya Ureno, hali ambayo imesambaratisha kabisa baadhi ya watu katika benchi la ufundi na sababu ikiwa ni ya huu Bwana Guardiola, yeye ndiyo amekuwa kama chanzo cha haya yote kutokea mara baada ya matokeo hayo kwa timu hiyo kupoteza.
    Kilichotokea ni jopo la madaktari wa timu hiyo akiwepo Daktari mkuu pamoja na idara yake nzima kuamua kujitoa katika wadhifa ndani ya timu hiyo kutokana na lawama walizozipata kutoka kwa Pep kuwa hawapo makini katika kazi yao na wao ndiyo chanzo cha matokeo kuwa mabaya kwa timu hiyo kufungwa na Fc. Porto.
    Kosa kubwa kubwa alilofanya Guardiola ni hali ya kupaniki kutokana na haya matokeo ambayo yanaipa nafasi ndogo ya Bayern Munich kuendelea kubaki katika harakati za kupambania taji la UEFA, ni swala ambalo limechukuliwa na daktari huyo kwa fikra na mawazo yakinifu kabisa kwani hakustahili kupata lawama hizo na ukiangali ani mtu ambaye amekaa na timu kwa muda mrefu sana na kilabu.
    Akiwa na miaka 72 hivi sasa Muller Wohlfahrt amekaa na timu hiyo kwa miaka 40, ni jambo la kushangaza sana kuona daktari amekuwa na timu kwa muda huo mrefu na leo akionekana kama kiraka kwenye timu jambo ambalo sio la kutarajia hata kidogo, kabisa. 
    Daktari wa timu ana wajibu wa kumweleza Mwalimu kama mchezaji yupo sawa kucheza na gilo atasema endapo mchezaji husika alikuwa na matatizo ya majeraha au anaumwa na Mwalimu wa timu ataamua kama kuna ulazimu wa kumchezesha au kutomchezesha, hapa ninaona kabisa Pep hajatenda jambo sahihi.
    Sioni kama Pep atabakia kuwa Kocha wa Bayern kwa msimu ujao na hili linaweza kutimia mapema endapo tu kama atatolewa katika mechi ya marudiano baada ya wiki mbili zijazo na Fc. 
    "Tenda wema siku zote na usingoje shukrani" hii ni kauli ambayo inatuonesha mema aliyoyafanya Daktari Bw. Muller Wohlfahr, kukaa miaka 40 katika timu huku ukiwa kama daktari mkuu na leo hii timu inafungwa halafu makosa ya ndani ya uwanja leo idara ya matibabu inakuja kupewa lawama ambazo hazihusiani na matokeo ya uwanjani.
    Kila la kheri huko utapoeleka Muller Wohlfahrt, siku zote penye nia pana njia na umeifanyia makubwa sana Bayern Munich na hakika watakukumbuka.
    Ahsanteni!!!!!!


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!