Na George Mganga
Balozi wa Uhispania nchini Tanzania, Luis
Cuesta amewapongeza wachezaji wa zamani wa
klabu ya Barcelona ya Uhispania kwa kufanya
ziara nchini Tanzania, huku akisema kuwa
udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona
umefungua milango ya ushirikiano kati ya nchi
hiyo na klabu hiyo kongwe duniani.
Akizungumza katika hafla ya jioni kwa ajili ya
wachezaji wa zamani wa FC Barcelona
iliyoandaliwa na Ubalozi wa Uhispania nyumbani
kwa balozi jijini Dar es Salaam, Cuesta amesema
kwamba ushirikiano wa Castle Lager na FC
Barcelona umefungua milango ya fursa
mbalimbali kwa Tanzania na klabu hiyo kongwe
ikiwemo ziara ya wachezaji wa zamani wa klabu
hiyo ambao walikuja nchini kucheza mechi ya
kirafiki na wachezaji wa zamani wa Tanzania.
Katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa Taifa
Dar es Salaam, wachezaji hao wa zamani wa
Barcelona walishinda 2-1 dhidi ya wachezaji wa
zamani wa timu ya taifa ya Tanzania.
Kwa upande wake, Baloziwa Uholanzi nchini
Tanzania, Jaap Frederiks ambaye naye
alihudhuria hafla hiyo kwa sababu ya wachezaji
wa Kiholanzi wanaochezea Barcelona alisema
kwamba amefurahi juu ya ziara hiyo na
anawapongeza Castle Lager kwa kuileta
Barcelona karibu na Afrika.
“Barcelona ni timu yenye wapenzi duniani kote.
Watanzania na nchi nyingine barani Afrika
watapata fursa ya kuwaona wachezaji wa timu
hii kubwa ikiwa ni jambo zuri na la
kihistoria,”alisema.
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Barcelona,
Johan Cruyff pamoja na gwiji wa Barcelona wa
zamani Luis Garcia ni kati ya walioudhuria hafla
hiyo.
0 comments:
Post a Comment