Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 February 2015
Thursday, February 05, 2015

“Tembo” watinga fainali AFCON.


Na Chikoti Cico
Timu ya taifa ya Ivory Coast maarufu kama “tembo” wametinga fainali ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuichapa timu ya taifa ya Jamhuri ya watu wa Congo (DR Congo) kwa magoli 3-1 kwenye hatua ya nusu fainali, katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Estadio de Bata.
Magoli ya Yaya Toure (dk 20), Gervinho (dk 41) na Kanon (dk 68) yalitosha kuipelekea Ivory Coast kwenye hatua ya fainali kwa mara ya tatu ndani ya miaka tisa kwenye michuano ya AFCON huku goli la kufutia machozi la DR Congo likifungwa na Mbokani kwa njia ya penati kwenye dakika ya 24 ya mchezo.
Kutokana na matokeo hayo Ivory Coast ambao ni mabingwa wa AFCON mwaka 1992 watacheza fainali dhidi ya Ghana ama wenyeji Guinea ya Ikweta katika mchezo mwingine wa nusu fainali utakaopigwa kwenye uwanja wa Estadio de Malabo leo usiku.
Vikosi vya timu zote mbili kwenye mchezo huo vilikuwa hivi: Kikosi cha DR Congo: Kidiaba, Mpeko, Kassusula, Zakuani, Kimwaki, Mbemba, Makiadi (Ndombe 79'), Mabwati (Kebano 69'), Bolasie, Bokila, Mbokani (Kabananga 61') Kikosi cha Ivory Coast: Gbhouo, Kanon, Toure, Bailly, Aurier, Tiene (Diarassouba 72'), Toure, Die, Gradel (Kalou 62'), Gervinho, Bony (Traore 90+2')

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!