Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 February 2015
Tuesday, February 03, 2015

Salah na Bertrand waondoka Chelsea.





Na Chikoti Cico


Winga wa Chelsea Mohamed Salah amepelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Fiorentina huku Chelsea wakimsajili Juan Cuodrado kutoka klabu hiyo ya nchini Italia kwa ada ya pauni milioni 27 huku mchezaji huyo akisaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu hiyo ya jijini London.

Salah mwenye umri wa miaka 22 anakuwa mchezaji wa pili kuondoka Chelsea kwenye dirisha dogo la usajili baada ya Andre Schurrler kuuzwa kwa klabu ya Wolfsburg kwa ada ya pauni milioni 24.

Pia klabu ya Chelsea imefanikiwa kumuuza moja kwa moja beki wa kushoto Ryan Betrand ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Southampton kwa ada ya pauni milioni 10.

Betrand amesaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu ya Southampton, mkataba utakaomuweka kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2019, kabla ya kusajiliwa kwa mkataba wa moja kwa moja Betrand tayari alikuwa ameshapelekwa mara saba kwa mkopo ndani ya miaka minane.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!