Goli kipa aisawazishia timu yake dakika za majeruhi
Na Florence George
Goli kipa wa timu ya soka ya Augsburg, Marwin Hitz amefunga goli na kisaidia timu yake ipate sare ya magoli 2-2 dhidi ya klabu ya Bayer Leverkusen katika mechi ya ligi kuu nchini Ujerumani.
Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Hitz tangu mwezi November baada ya kupona majeraha yake ya enka ,alifunga goli hilo baada ya timu yake kupata kona katika dakika za mwishoza mchezo huo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswisi alipiga shuti akiwa umbali wa mita sita baada ya mabeki wa Leverkusen kushindwa kuondoa mpira katika eneo la hatari.
Kwa mujibu wa rekodi za ligi kuu nchini Ujerumani Marwin Hitz amekuwa goli kipa wa tatu kufunga goli ndani ya mchezo tofauti na penati na kuisaidia timu yake kushika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi hiyo.
0 comments:
Post a Comment