Barcelona yabanwa na Malaga ,Athletico yashinda.
Na Florence George
Baada ya kucheza michezo 11 bila kupoteza hatimae klabu ya soka ya Fc Barcelona ya nchini Hispania imekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa timu ya Malaga katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania uliochezwa katika dimba ya Camp Nou.
Katika mchezo huo ambao asilimia kubwa ulimilikiwa na wenyeji ambao walijikuta wakifungwa goli katika dakika ya saba tu ya mchezo kufuatia makosa ya beki Dani Alves kurudisha mpira kwa goli kipa na kunaswa na Jiménez López na kufunga goli hilo lililodumu hadi dakika 90 zinaisha uwanjani.
Barcelona waliingia uwanjani wakiwa wamefunga magoli 42 katika ushindi wake wa mechi za hivi karibuni huku nyota wao Lionel Messi akiwa amesaidia kupatikana kwa magoli 10 lakini walishindwa kusawazisha goli hilo la mapema .
Malaga imekuwa timu ya kwanza kutoruhusu kufungwa goli katika michezo miwili dhidi ya Barcelona tangu Getafe ilipofanya hivyo msimu wa 2007/2008 kwani katika mchezo wa kwanza uliochezwa mwezi September mwaka jana uliisha kwa suluhu (0-0).
Kwa matokeo hayo sasa Barcelona inaendelea kubaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 56,pointi moja nyuma ya vinara Real Madrid ambao wanashuka dimbani leo kumenyana na Elche.
Kwa upande mwingine timu ya Athletico Madrid imefanikiwa kushinda magoli 3-0 dhidi ya Almeria huku Mario Mandzukic akianza kuifungia Athletico dakika ya 13 kwa mkwaju wa penati kabla ya Antoine Griezmann kufunga magoli mawili katika dakika ya 20 na 29.
Athletico Madrdid imefikisha pointi 53 katika michezo 24 iliyocheza na kutoa presha kwa Barcelona iliyonafasi ya pili huku ikiwa nyuma ya pointi nne dhidi ya Real Madrid iliyo nafasi ya kwanza.
Barcelona inajiandaa kucheza na Manchester City siku ya jumanne katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa kombe la Klabu bingwa barani Ulaya(UEFA) mchezo utakaochezwa katika dimba ya Etihad jijini Manchester nchini Uingereza.
0 comments:
Post a Comment