Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 January 2015
Thursday, January 01, 2015

Uchambuzi: Tottenham Hotspur vs Chelsea


Na Chikoti Cico

Mechi inayosubiriwa kwa hamu kwenye kwenye pazia la mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini Uingereza ni kati ya Tottenham Hotspur dhidi ya Chelsea mchezo unaojulikana kama “London Derby” ambao utapigwa kwenye uwanja wa White Hart Lane.

Tottenham baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Manchester United kwenye mchezo uliopita wa siku ya “boxing day” na kufikisha alama 31 huku wakishika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi wanatarajiwa kupigania kupata alama tatu muhimu ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuingia “top four”.

Kocha wa Spurs Mauricio Pochettino kuelekea mchezo huo hana wachezaji majeruhi hivyo anatarajiwa kukibadili kikosi chake huku Kyle Walker, Danny Rose, Erik Lamela na Aaron Lennon ambao walikuwa majeruhi wanaweza kurejea kikosini bada ya kupona na kuwa fiti kuikabili Chelsea.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha Spurs wamefungwa michezo minne na kutoka sare michezo mitano katika michezo tisa iliyopita dhidi ya Chelsea.

Wakati huo huo Spurs wana rekodi ya kupata ushindi wa magoli 2-1 mara sita kwenye msimu huu wa ligi huku wakiwa hawajapata matokeo mengine ya magoli mara mbili zaidi.

Kikosi cha Pochettino kinaweza kuwa hivi: Lloris; Walker, Fazio, Vertonghen, Davies; Mason, Bentaleb, Lamela, Eriksen, Chadli; Kane

Vinara wa ligi ya Uingereza timu ya Chelsea wakiwa na alama 46 kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu na kuendelea kujikita kileleni.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho pia hana wachezaji ambao ni majeruhi hivyo anaweza kubadili kikosi cha timu hiyo hasa ikizingatiwa kwamba kuna mchezo wa kombe la FA dhidi ya Watford siku ya Jumapili.

Takwimu zinaonyesha Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba amehusika kwenye magoli tisa katika michezo tisa dhidi ya Spurs huku akifunga magoli manne na kutoa pasi tano za magoli.

Pia kiungo wa timu hiyo Cesc Fabregas akihusika kwenye magoli 10 katika michezo nane dhidi ya Spurs huku akitoa pasi nane za magoli na kufunga magoli mawili.

Chelsea pia wana rekodi nzuri kwenye michezo ya siku ya mwaka mpya kwani katika michezo nane iliyocheza tarehe moja ya Januari imeshinda michezo sita na kutoka sare michezo miwili.

Kikosi cha Chelsea kinaweza kuwa hivi: Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Fabregas, Matic, Willian, Oscar, Hazard; Costa

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!