Barcelona wanahitaji ushindi tu mbele ya Atletico Madrid leo.
Na Oscar Oscar Jr
Majira ya saa 5:00 usiku leo utapigwa mchezo wa ligi kuu Hispania ambao utawakutanisha Barcelona dhidi ya mabingwa watetezi Atletico Madrid kwenye dimba la Camp Nou mahali ambapo zaidi ya mashabiki 98,000 watakuwa uwanjani hapo kushuhudia mpambano huo.
Licha ya Ushindi wa bao 5-0 dhidi ya timu ya Elche kwenye kombe la Mfalme, bado hali si swari kwenye klabu hiyo baada ya kocha Luiz Enrique kutokuwa na mahusiano mazuri na wachezaji wenye majina makubwa akiwemo Mfalme wa Ballon D'or, Lionel Messi.
Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid, vijana wa Atletico Madrid watakuwa na kiu ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo hasa ukizingatia kuwa, katika mechi sita za hivi karibuni wamekuwa wakiwabania Barcelona kuondoka na alama tatu.
Barcelona ambao mchezo uliopita wa ligi kuu walifufungwa na Real Sociedad, wanaonekana kuwa na nafasi ya kufanya vizuri endapo kocha Luiz Enrique atakubali kuwaanzisha Lionel Messi, Neymar na Luiz Suares ili kuweza kuwatia kwenye presha vijana na kocha Diego Semeoni.
Barcelona ambao wanakamata nafasi ya pili wakiwa na alama 38 sambamba na Atletico Madrid, wangependa kupunguza mwanya wa alama kati yao na vinara Real Madrdi ambao wamefikisha alama 42 baada ya hapo jana kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Espanyol.
Atletico bado wanaonekana kuwa moto baada ya wachezaji wao wapya kuanza kuingia kwenye mfumo wa timu na kufanaya vizuri. Ushindi katika mchezo wa leo, utawafanya mabingwa hao watetezi kuweza kutimiza alama 41 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.
Mashabiki wa Barcelona tayari wameanza kumzomea kocha Enrique na endapo watapoteza mchezo wa leo au endapo kocha atawaanzishia benchi Messi na Neymar, kuna uwezekano hali ya mgogoro ikaongezeka na kumuweka kocha huyo kwenye mazingira ya kupigwa chini.
0 comments:
Post a Comment