Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 January 2015
Saturday, January 10, 2015

Real Madrid yaichapa Espanyol


Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye mabingwa wa Ulaya na Dunia klabu ya Real Madrid imerejea kwenye mbio zake za ushindi baada ya hapo jana kujipatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Espanyol licha ya kucheza kwa zaidi ya dakika 40 wakiwa 10 uwanjani.

Mabao matatu kutoka kwa Gareth Bale, James Rodriguez na Nacho yalitosha kuwafuta machozi vijana hao wa kocha Carlo Ancelotti ambaye ametoka kufungwa mfululizo na timu za Valencia na Atletico Madrid.

Kufuatia ushindi huo, Real Madrid wanatimiza alama 42 kufuatia kushuka dimbani mara 17 huku wakiwa wamepoteza michezo mitatu na hakuna sare hata moja waliyopata msimu huu. 

Mchezo huo ulimshuhudia beki wa kushoto wa timu hiyo Fabio Coentrao akipewa kadi nyekundu na kuwafanya wenzie kucheza muda mrefu wakiwa pungufu.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!