Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 January 2015
Thursday, January 01, 2015

Spurs yaisambaratisha Chelsea


 Na Oscar Oscar Jr

Harry Kane kwa mara nyingine aliendelea kuitendea haki nafasi ya ushambuliaji kwenye kikosi cha TottenHam Hotspurs baada ya kuonyesha kiwango kizuri huku akifunga mabao mawili kwenye mchezo uliomalizika kwa Spurs kuichapa Chelsea kwa mabao 5-3.

Diego Costa alikuwa wa kwanza kufunga kwa upande wa Chelsea lakini kibao kiligeuka na kuwa dhahama kwa watoto wa kocha Jose Mourinho. Magoli ya Spurs yalifungwa na Harry Kane aliyefunga mara mbili huku Rose, Townsend 45′ (pen) na Chadli wakifunga mengine.

Kwa upande wa Chelsea, magoli yao yalipatikana kupitia Diego Costa, Eden Hazard na John Terry. Kichapo hicho sasa kimeongeza upinzani kwa sababu timu ya Manchester City jana ilipata ushindi wa mabao 3-2 Sunderland ambapo nao wametimiza alama 46 ambazo ni sawa na walizonazo Chelsea.

Spurs ambao sasa wamefikisha alama 34, wamepanda kwenye msimamo wa ligi kuu hadi nafasi ya tano na kuwashusha Arsenal ambao jana waliweza kuchezea kichapo cha mabao 2-0 ugenini mbele ya Southampton ambao wanakamata nafasi ya nne.

Harry Kane ni moja kati ya washambuliaji wachanga ambao wameanza kuingia kwenye vichwa vya wapenzi wa mchezo huo na hasa mashabiki wa Spurs. 

Kijana huyo tayari amefunga msimu huu mabao 17 kwenye mashindano yote na ni mchezaji mmoja tu Sergio Kun Aguero wa Manchester City ndiyo mwenye magoli mengi kuliko yeye. 

Akizungumza mara baada ya mchezo huo ambao Spurs walitawala kwa asilimia 46 kwa mujibu wa bbc Sports, kocha Mouricio Pochettino amekiri kuwa walistahili kushinda na pongezi ziwaendee wachezaji wake na mashabiki ambao walisimama nyuma ya timu muda wote.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!