Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 January 2015
Thursday, January 01, 2015

Gunners wachezea kichapo cha tano.


Na Oscar Oscar Jr

Magoli mawili yaliyofungwa na Saido mane na Dusan Tudic yalitosha kuzamisha jahazi la kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza uliopigwa ndani ya dimba la St. Marrys huku vijana wa kocha wa Kidachi, Southampton wakiibuka na ushindi uliowafanya wabakie kwenye nafasi ya nne.

Makosa ya golikipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny yaliweza kurahisisha kazi kwa Southampton kuweza kuisambaratisha timu hiyo ambayo kutokana na mwendo wake wa kusua sua, mashabiki na wanachama wamekuwa wakiuponda ufundi wa Arsene Wenger huku tatizo sugu la kikosi hicho likiwa ni kukosa kikosi kipana chenye nguvu.

Arsenal wanaendelea kubakia na alama 33 ambazo zinawatupa hadi kwenye nafasi ya sita na kuanza kuwa kwenye wakati mgumu wa kutafuta tena kuingia kwenye timu nne za juu. 

Ni mara chache sana kwa timu pinzani kutawala mchezo inapocheza na Arsenal na hata jana, Gunners walitawala kwa asilimia 59 huku mashuti sita yakilenga golini lakini, hakuna goli walilopata.

Kwa upande wa pili, mahasimu wa Arsenal timu ya Tottenham HotSpurs waliweza kuwa na mwanzo mzuri wa mwaka baada ya kuwachapa Chelsea kwa mabao 5-3 kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la White Hart Lane na kuifanya timu hiyo ya kocha Mouricio Pochettino kuinyemelea nne bora baada ya kusogea hadi nafasi ya tano.

Hiki kinakuwa kichapo cha tano kupewa kwa timu ya Arsenal msimu huu huku ikionekana kushinda mara tisa na kutoka sare kwenye michezo sita. Kwa upande mwingine, Manchester United walitoka sare na Stoke City ya bao 1-1.

Magoli katika mchezo huo yalifungwa na Rayan Shawcross kwa upande wa Stoke City na Radamel Falcao akifunga kwa upande wa Manchester United na kuwafanya United kusalia kwenye nafasi ya tatu wakiwa na alama 37.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!