Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 August 2014
Saturday, August 02, 2014

Ligi kuu Tanzania bara imepoteza mechi moja ya watani wa jadi.

Na Oscar Oscar Jr

Uwanja wa Kambarage pale Mkoani Shinyanga ndipo wanapopatikana timu ya Stand United. Kama zingeruhusiwa kupanda na kucheza ligi kuu timu mbili kutoka kwenye kila kundi, basi tungeshuhudia mechi nyingine yenye mvuto ya watani wa jadi "Derby" kati ya Stand United dhidi ya Mwadui fc msimu ujao. 

Mwadui fc walifikisha alama 31 huku wapinzania wao, Stand United wakifikisha alama 32 na hivyo Mwadui hawakufanikiwa kupanda daraja.

Taarifa za uhakika ni kwamba Stand United wanajiandaa kucheza mechi 11 za maandalizi kuelekea kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara septemba 20 mwaka huu na kati ya hizo, watajipima nguvu na timu mbili kutoka nchini Kenya na nyingine mbili kutoka Uganda. 

Kutokana na ubora wa timu kama Mbeya City, Azam, Simba na Yanga, viongozi wa United wanadhani ni bora wachezaji wakaanza kuzoea kwa kucheza na timu za nje ya nchi kwanza.

Timu za ligi kuu ni lazima zitarajie upinzani wa hali ya juu kutoka kwa Stand United hasa kwenye michezo ya  awali kwa sababu, United wanaonekana ni timu ngumu sana kufungwa mechi za mwonzoni mwa ligi. 

Wakiwa daraja la kwanza kwenye michezo minne ya awali ya ligi, walishinda michezo mitatu, wakatoka sare mchezo mmoja na hakuna mchezo wowote waliopoteza huku wakifunga mabao matano na kuruhusu kufungwa bao moja pekee.

Stand United na Mwadui fc ni watani wa jadi na mechi baina ya pande hizi mbili, huwa na mvuto wa kipekee kwa sababu timu moja (Mwadui fc) inaringia nguvu kubwa ya pesa huku nyingine (Stand United) ikijivunia nguvu kubwa ya mashabiki.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!