Na Chikoti Cico
Kaka wa kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Serbia Nemanja Matic aitwaye Uros Matic amkacha mdogo wake huyo na kuamua kuichezea timu ya taifa ya Macedonia huku akimwacha Nemanja akiichezea timu ya taifa ya Serbia.
Uros ambaye ana miaka 24 huku akicheza nafasi ya kiungo mshambuliaji aliichezea mechi saba timu ya taifa ya Serbia chini ya umri wa miaka 19 kabla ya kuamua kuichezea timu ya wakubwa ya taifa la Macedonia.
Hivi karibuni mchezaji huyo alitembelea makao makuu ya chama cha soka cha Macedonia na kupiga picha akiwa na jezi namba tisa ya timu ya taifa hilo huku akiwa na Raisi wa chama hicho cha soka cha Macedonia Ilco Georgioski.
Georgioski aliuambia mtandao wa chama hicho kwamba “Matic alivuta umakini wetu kwa mchezo mzuri akiichezea timu ya NAC Breda na atakuwa bonasi kwenye kikosi.
Atakuwa tayari kuungana nasi mapema akikamilisha makaratasi ya kubadilisha pasi yake ya michezo na tunategemea kuwa nae kwenye timu ya taifa”
Macedonia inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi C ikiwa na alama tatu katika michezo minne ya kuwania nafasi ya kufuzu kwa michuano ya mataifa ya Ulaya kwa mwaka 2016 maarufu kama “Euro 2016”.
Slovakia wanaongoza kundi hilo wakiipita Macedonia kwa alama tisa huku pia Hispania na Ukraine wakiipita timu hiyo kwa alama sita, mchezo unaofata wa Macedonia utakuwa ni dhidi ya Belarus utakaochezwa tarehe 27 ya mwezi Machi.
0 comments:
Post a Comment