Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 January 2015
Sunday, January 11, 2015

Samatta mchezaji bora kwa mwaka 2014.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya nchini Kongo Mbwana Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2014 kutoka mtandao wa “Goal.com”.

Samatta ameshinda tuzo hiyo baada ya kupata asilimia 48 ya kura zilizopigwa kati ya Desemba 1-5, 2014 na kuwapita Mrisho Ngasa, Jonas Mkude, Salum Abubakar na Thomas Ulimwengu katika mchakato wa kura hizo zilziopigwa na mashabiki mbalimbali wa soka.

Akiongea baada ya kupokea tuzo ambayo ni kwa mara ya kwanza imetolewa na mtandano huo wa habari za michezo, Samatta alisema ““Najisikia furaha sana kuwa mshindi wa tuzo hiyo inayotolewa kwa mara ya kwanza Tanzania na Mtandao wenu wa Goal kwani inaonyesha ni kiasi gani mnathamini jitihada zangu na inanipa hamasa yakuzidi kujituma na kuendelea kupokea tuzo hiyo kila mwaka”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!