Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 January 2015
Sunday, January 11, 2015

Bonny sasa amesajiliwa rasmi.


Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye klabu ya Manchester City imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Swansea, Wilfredy Bonny. 

Mshambuliaji huyo ambaye amefunga mabao 20 kwa kalenda ya mwaka 2014, kwa sasa yuko barani Afrika kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.

Mshambuliaji huyo alianza kuwindwa na klabu hiyo baada ya washambuliaji wa Manchester City Kun Aguero, Eden Dzeko na Steven Jovetic kuwa majeruhi mara kwa mara. 

Ujio wa Bonny utamuongezea nguvu kocha Manuel Pellegrini kuweza kupigana kuhakikisha wanatetea ubingwa wao.

Bonny anadaiwa kuwagharimu Manchester City Pauni 30M na hii inakuwa ni rekodi ya uhamisho kwa klabu hiyo ya Wales Swansea City ambapo mchezaji aliyekuwa amenunuli kwa bei kubwa kutoka kwenye klabu hiyo ni Joe Allen ambaye alinunuliwa na Liverpool 2012 kwa Pauni 15M.

Wilfredy Bonny ambaye alinunuliwa kutoka klabu ya  Vitesse Arnhem ya huko nchini Uholanzi, mchezaji huyo aliwagharimu Swansea City Pauni 12M. Manchester City kwa sasa wanakamata nafasi ya pili wakiwa na alama 47 huku Chelsea wakiwa kileleni na alama 49.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!