Marco Reus kuelekea klabu ya Chelsea.
Na Oscar Oscar Jr
Vinara wa ligi kuu Uingereza timu ya Chelsea, wameamua kuanza kumfukuzia kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund, Marco Reus.
Mourinho anadaiwa kumtaka mshambuliaji huyo kufuatia Andre Schuerrle kushindwa kuingia kwenye mfumo wa kocha huyo raia wa Ureno.
Marco Reus ambaye amekuwa nje kwa muda kutokana na majeruhi yaliyokuwa yanamuandama, kwa sasa amerejea kwenye mazoezi na anaendelea kujifua kipindi hiki ambapo ligi ya Bundesliga imesimama.
Mshambuliaji huyo amekuwa akitajwa kujiunga na timu za Arsenal, Liverpool na Real Madrid kwa nyakati kadhaa lakini taarifa ya leo zimemtaja kama mbadala ya Schurrle pale Chelsea.
Kuonyesha kuwa Schurrle maisha yake ndani ya Stanfford Bridge yanaweza yakawa yamefikia mwisho, Chelsea wamejipanga pia kumfukuzia kiungo mshambuliaji wa Fiorentina, Juan Cuadrado ambaye amewahi pia kuhusishwa na klabu ya Manchester United.
Kama mmoja wa viungo hawa washambuliaji atajiunga na Chelsea, ni wazi kuwa timu hiyo itazidi kuwa tishio na kuondoa utegemezi kwa winga ya kushoto ambapo amekuwa akicheza Eden Hazard na kutoa mchango mkubwa kwenye kikosi hicho ambacho kinaongoza ligi kwa sasa wakiwa na alama 49 huku Manchester City wakiwafuatia wakiwa na alama 47.
0 comments:
Post a Comment