Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 January 2015
Friday, January 09, 2015

Sakata la David De Gea katika sura mpya.


Na Oscar Oscar Jr

Habari kuhusu hatima ya Golikipa namba moja wa Manchester United, David De Gea kila siku inazidi kuchukuwa sura mpya huku mkataba wa kipa huyo ukitajwa kumalizika mwaka 2016. 

Habari zilizotoka leo zinadai kuwa, Real Madrid wamemuweka kipa huyo kwenye mpango wa kuwa kipa namba moja huku kocha pia wa Hispania, Vicente del Bosque akimuhitaji kipa huyo kuchukuwa nafasi ya mkongwe, Iker Casillas.

Manchester United pamoja na kumsajili Victor Valdes kama kipa namba mbili kwa mkataba wa miezi 18, bado wameendelea kuripotiwa kumuwinda kipa Mdachi ambaye anakipiga na klabu ya Newcastle United, Tim Krul. 

Kitendo cha Manchester United kuanza kutafuta kipa mwingine licha ya kuwa tayari wamempata Victor Valdes ni ishara kuwa hawana uhakika kama wataendelea kuwa na De Gea ambaye ameonekana kuwa moja ya wachezaji bora wa klabu hiyo msimu huu.

Manchester United ambao wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza, mpaka sasa wameruhu magoli 20 kutinga kwenye nyavu zao ambako De Gea ndiye shujaa wa lango hilo wanajianda kucheza na Southampton siku ya Jumapili kwenye dimba la Old Trafford.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!