Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 January 2015
Friday, January 09, 2015

Mafundi wa Gunners wamerejea dimbani.


Na Oscar Oscar Jr

Wacheza wa Arsenal, Mesut Ozil, Aaron Ramsey na Methieu Flamini wote wamerejea kwenye kikosi cha kwanza na kufanya mazoezi. 

Akizungumza kuelekea mchezo wa siku ya Jumapili dhidi ya Stoke City, kocha Arsenal mzee Wenger amethibitisha hilo na hii ni habari njema kwa mashabiki wa Gunners.

Ozil alikuwa nje tangu mwezi Octoba mwaka jana huku Ramsey akikosekana tangu kuanza kwa mwezi Desemba. Kurudi kwa wachezaji hao kutapunguza utegemezi wa timu hiyo ambayo kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakimtegemea Alexies Sanchez.
\
Kurejea kwa wachezaji huo kwenye kikosi cha Arsenal, kutaleta manufaa hasa ukizingatia timu hiyo inakabiliwa na upinzani wa hali ya juu kutoka timu za Manchester United, Tottenham, Southampton na West Ham United katika mbio za kumaliza kwenye moja kati ya nafasi nne za juu.

Alipoulizwa swali kocha wa timu hiyo kama kunauwezekano wa Mesut Ozil kuanza kwenye mchezo wa siku ya Jumapili, Wenger alijibu kuwa hana uhakika na pengine siku ikifika ndipo atakapoamua kama aanze kwenye kikosi cha kwanza au atokee benchi.

Arsenal kwa sasa wanakamata nafasi ya sita wakiwa na alama 33, watamkosa mshambuliaji Danny Welbeck ambaye bado ni majeruhi lakini Olivier Giroud atarejea baada ya adhabu yake ya kadi nyekundu kumalizika.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!