Na Chikoti Cico
Hayo ni maneno ya nahodha na kipa wa timu ya Real Madrid, Iker Casillas wakati akiongea na redio ya COPE ya nchini Hispania. Casillas ni moja ya wachezaji ambao hawakuwa na mahusiano mazuri na Jose Mourinho wakati akiifundisha timu hiyo kati ya mwaka 2010 na 2013.
Akiongea na Redio hiyo Casillas alisema “Ancelotti ni bora zaidi kuliko Mourinho, nikiwa na Mourinho nlikuwa na uhusiano wa upendo na chuki, muda wake hapa sikuzungumza nae tukiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, na hata sijafikiria kuzungumza nae kwasasa wakati tayari anafundisha timu nyingine na nikiwa na timu yangu”.
“Itakuwa ni kuangalia mambo yangu na woga mdogo kwa upande wangu, namtakia mambo yamwendee vizuri, katika muda alipokuwa Real Madrid alishinda vikombe na unatakiwa kumpa shukrani.
Kama nikikutana nae kesho nitampa mkono halafu itakuwa ni kwa upande wake kama ataushika, nafikiri ataushika”.
Akiongelea uhusiano wake na Xabi Alonso hasa baada ya Alonso kusema kuwa kipa bora duniani ni Manuel Neuer ambaye anacheza nae Bayern Munich kuliko yeye, Casillas alisema “hainivutii kwa Xabi Alonso anachosema, katika miaka ya karibuni uhusiano wetu haukuwa unatosha”
0 comments:
Post a Comment