Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 January 2015
Thursday, January 15, 2015

Robben kuzeekea Bayern Munich


Na Chikoti Cico

Winga wa timu ya taifa ya uholanzi na klabu ya Bayern Munich Arjen Robben amesema ataendelea kuichezea klabu hiyo mpaka mwili wake utakaposhindwa kufanya hivyo ikiwa kama ni baada ya mwaka mmoja ama miaka 10 ijayo.

 Mchezaji huyo ambaye aliwahi kuzichezea klabu za Chelsea na Real Madrid kabla ya kusajiliwa na Bayern Munich mwaka 2009, alichagulia kati ya wachezaji 11 kwenye kikosi bora cha FIFA kwa mwaka 2014 yaani “2014FIFPro World X1” kilichotajwa siku ya Jumatatu wakati wa hafla ya tuzo ya Ballon d’Or mjini Zurich.

Robben akiongelea kuhusu kama atastaafu karibuni alisema “naulizwa mara nyingi kwasasa lini ntamaliza kucheza soka kwasababu nazeeka, nimepumzika katika hilo, mwili ukifanya kazi na nafurahia ntaendelea, labda mwaka mmoja, miaka miwili ama labda miaka 10, jinsi unavyozeeka ndivyo unavyoujua mwili wako vizuri”.

Pia Robben ambaye mara nyingi amekuwa akimsifia kocha wa Bayern Munich Pep Guadiola, alimwongelea kocha huyo na kusema “kwa Pep, nilikuwa na hisia nzuri tokea mwanzoni, alijaribu kuiboresha timu lakini pia kumboresha kila mchezaji, nina shukrani kwamba nimefanya kazi nae kwa miezi 18 kwasasa.

Amenifanya mimi kuendelea na namshukuru kwa hilo”.
Aliendelea kusema “tumecheza katika mifumo mbalimbali na hilo linafanya uendelee kama mchezaji, nimekuwa na nafasi tofauti tofauti napenda hilo, inafurahisha kwenda kwenye kikao cha mbinu na kujifunza jinsi ya kucheza nafasi mpya pia kuwashtukiza wapinzani”

Wakati huo huo klabu ya Bayern Munich inatarajiwa kurejea dimbani kwenye ligi ya Bundesliga mwisho wa mwezi wa kwanza kucheza na timu ya Wolfsburg baada ya mapumziko ya wakati wa baridi katika mfululizo wa ligi hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!