Diego Costa na Chelsea wako kileleni.
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya kujipatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United, watoto wa Mourinho timu ya Chelsea imeweza kujipatia ushindi wake wa 10 nyumbani na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu huku wakiwazidi Manchester City kwa alama mbili ambao wametoka sare ya 1-1 dhidi ya Everton.
Oscar na Diego Costa waliwaweka Chelsea mbele kwa mabao yao na sasa Diego Costa anakuwa kinara wa mabao ligi kuu baada ya kufunga bao lake la 15 msimu huu.
Ushindi huo unawafanya Chelsea kufikisha alama 49 huku Manchester City wakitimiza alama 47 kwenye nafasi ya pili.
Katika mchezo huo ambao Chelsea waliweza kutawala kwa asilimia 63, kipindi cha kwanza kilishuhudia Newcastle United wakiwa imara huku mpira mmoja uliyopigwa na Moussa Sissoko ukienda na kugonga mwamba wa lango la Chelsea .
Huu ni ushindi wa 15 kwa Chelsea msimu huu huku wakiwa wametoka sare mara nne na kupoteza mechi mbili kati ya michezo 21 walioshuka dimbani msimu huu.
Chelsea ambao mchezo uliopita walifungwa na Spurs bao 5-3, wanaonekana kurejea kwenye wimbi lao la ushindi ambapo msimu huu wamekuwa wakitajwa kama timu tishio.
0 comments:
Post a Comment