Na Oscar Oscar Jr
Hatimaye mabingwa wa Dunia kwa ngazi ya vilabu timu ya Real Madrid, wameweza kupokea kichapo kwa mara ya tatu kwenye La Liga msimu huu na kusitishwa kwa rekodi yao ya kucheza mechi 22 bila kupoteza mcheza wowote wa ushindani.
Goli lililofungwa na Nicolas Otamendi wa Valencia kwenye dakika ya 65, lilitosha kuwapatia ushindi vijana wa Valencia huku wakipewa sifa kwa kitendo chao cha kutoka nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Christiano Ronaldo kwa mkwaju wa penati na kurejea kutwaa pointi tatu kwenye mchezo huo.
Huu ni ushindi wa pili kupata kwenye mechi 11 walizokutana na Real Madrid wakiwa kwenye dimba la Mestalla na sasa wanaendelea kufufua matumaini ya kumaliza kwenye moja ya nafasi nne za juu.
Valencia kwa ushindi huo wanatimiza alama 34 na kuzidiwa alama moja tu na Atletico Madrid ambao wanakamata nafasi tatu wakiwa na alama 35.
Bao la Christiano Ronaldo kwenye mchezo huo, linakuwa la 26 katika mechi 16 Real Madrid walizocheza msimu huu na anaendelea kuongoza mbio za kutwaa kiatu cha ufungaji bora kwa mara nyingine.
Matokeo hayo yanaendelea kuwabakiza Real Madrid kileleni wakibaki na alama 35 huku wakisubiri matokeo ya Barcelona ambao wanashuka dimbani majira ya saa 5:00 Usiku leo ugenini dhidi ya Real Sociedad na kama watafanikiwa kupata ushindi, watapanda kileleni na kuwashuka Real Madrid kwenye nafasi ya pili japo wanamchezo mmoja mkononi.
0 comments:
Post a Comment