Liverpool na dirisha la Usajili.
Na Oscar Oscar Jr
Mshambuliaji wa klabu ya Olympic Lyon, Alexandre Lacazette ameruhusu klabu zinazomuhitaji kuanza kumfukuzia baada ya kusema kuwa yuko tayari kucheza ligi kuu nchini Hispania au Uingereza.
Klabu ya Liverpool na Arsenal zinaonekana kupigana vikumbo baada ya kuhitaji mshambuliaji mahiri hasa ukizingatia kuwa mshambuliaji huyo ndiye anayeongeza kwa kupachika magoli Ufaransa mpaka sasa akiwa na magoli 11.
Kumekuwa na habari za klabu ya Olympiakos kumuhitaji kwa mkopo mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli huku wakiwa tayari kumlipa mshahara wote mshambuliaji huyo. Mario amegoma na kudai kuwa hana mpango wa kuondoka Liverpool kwenye dirisha hili la usajili.
Mshambuliaji wa Uingereza na klabu ya Manchester City, James Milner mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu huu na leo kumekuwa na taarifa kuwa, klabu ya Liverpool inataka kumsaini mchezaji huyo hasa ukizingatia kuwa, ameonyesha kiwango kizuri sana siku za hivi karibuni kila alipopewa nafasi.
Kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Fernando Suso ametajwa kutaka kujiunga na timu ya Ac Millan kwa mkataba wa miaka minne huku mshambuliaji Rickie Lambert, ametajwa kutaka kujiunga na klabu ya Crystal Palace.
0 comments:
Post a Comment