Manchester United na dirisha la Usajili.
Na Oscar Oscar Jr
Manchester United wanajiandaa kupeleka ombi rasmi la kumuhitaji beki wa Kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund, Mats Hummels huku klabu hiyo ikiandaa kitita cha Pauni 35M.
Pamoja na jitihada hizo za kikosi cha kocha Loius Van Gaal kujaribu kumaliza kwenye moja ya nafasi nne za juu, baba mzazi wa mchezaji huyo amedai kuwa beki huyo hawezi kuondoka Dortmund katika dirisha hili.
Kutokana na timu hiyo kutaka kumalizana na mshambuliaji Radamel Falcao, maongezi hayo yanadaiwa kuchelewesha kuongezwa mkataba kwa Golikipa David De Gea.
De Gea ambaye anasakwa na Real Madrid, anadaiwa kusubiri mazungumzo na United ambapo mkataba wake mpya unatajwa kumfanya awe analipwa Pauni 140,000 kwa wiki ambayo ni mara mbili na anacholipwa kwa sasa.
Baada ya klabu hiyo inayokamata nafasi ya tatu kwenye ligi kuu kumuwania kiungo wa klabu ya As Roma, Kevin Strootman kwa muda mrefu, kumeibuka habari kuwa mchezaji huyo anataka kuendelea kubakia na klabu yake na hana mpango wa kwenda Old Trafford.
Katika habari kubwa ni timu za Manchester United, Chelsea na Arsenal kuhusishwa na usajili wa mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suares ambaye amesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea klabu ya Liverpool kutokana na hali kuwa tete ndani ya klabu ya Barcelona ambako Lionel Messi pia anatajwa kutka kuondoka.
0 comments:
Post a Comment