Na Chikoti Cico
Mshambulijai wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid Christiano Ronaldo amenyakua tena tuzo ya mchezaji bora duniani maarufu kama “Ballon d’Or”akiwashinda Lionel Messi na Manuel Neur, hii ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 amechukua tuzo hiyo baada ya kuifungia timu ya Real Madrid jumla ya magoli 56 katika michezo 51 huku klabu hiyo ikichukua makombe manne katika kalenda ya soka kwa mwaka 2014.
Real Madrid imechukua kombe la Mfalme (Copa del Rey), Kombe la ligi ya mabingwa Ulaya, Kombe la UEFA (UEFA Super Cup) na kombe la klabu la dunia kwa klabu (Club World Cup).
Ronaldo akiongea baada ya kupokea tuzo hiyo iliyotolewa na Thierry Henry alisema “ninamwona Mama yangu, familia yangu, ningependa kuwashukuru wote ambao walinipigia kura, kocha wangu, wachezaji wenzangu, Raisi wa klabu yangu”.
“Umekuwa ni mwaka usiosahaulika, kushinda tuzo hii, tuzo ya aina hii ni kitu cha pekee na ambacho ninaweza kusema ni nataka kuendelea kufanya kazi kama ninavyofanya, kujaribu kuendelea kwaajili ya vikombe zaidi, binafsi na kama timu, kwaajili ya Mama yangu, Baba yangu aliyejuu akiangalia hapa na mwanangu”
aliendelea kusema “ninataka kuwa bora siku zinavyoenda, nataka kusema kwa wareno wote kwamba kamwe sikufikiri ningeweza kushinda tuzo hii mara tatu tofauti, hakika ni kitu ambacho kipo mara zote kwangu, nataka kuwa moja ya wachezaji bora wa muda wote na hili linahitaji vingi hivyo ningependa kuwashukuru ninyi kwa usiku huu. BOOM!”
0 comments:
Post a Comment