Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 January 2015
Monday, January 12, 2015

Low awabwaga Ancelotti na Simeone.


Na Chikoti Cico

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low awabwaga kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti na kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone kwenye tuzo ya kocha bora wa Dunia wa FIFA kwa mwaka 2014.

Low ametangazwa kama kocha bora wa dunia wa FIFA baada ya kuiongoza timu ya taifa ya Ujerumani kunyakua kombe la Dunia kwa mwaka 2014 kwa kuifunga timu ya Argentina kwenye mchezo wa fainali kwa goli 1-0 katika fainali zilizofanyika nchini Brazili mapema mwezi wa saba mwaka jana.

Low mwenye umri wa miaka 54 baada ya kupokea tuzo hiyo iliyowasilishwa na kocha wa zamani wa Bayern Munich Ottmar Hitzfeld alisema “hii ni heshima kubwa kwangu kupokea tuzo hii baada ya mafanikio makubwa ya 2014, hii imenogesha kombe la Dunia. Hii haichukuliwi kwangu kuwa mali yangu lakini naichukua kwaniaba ya wengine”.

Kocha huyo wa Ujerumani ambaye alianza kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo kama kocha mkuu mwaka 2006 aliiwezesha Ujerumani kushika nafasi ya tatu kwenye fainali za kombe la Dunia kwa mwaka 2010 zilizofanyika nchini Afrika ya Kusini kabla ya kunyakua kombe hilo mwaka uliopita nchini Brazili.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!