Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 January 2015
Thursday, January 08, 2015

Mchezaji bora wa Afrika.


Na Oscar Oscar Jr

Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Uingereza ya Manchester City, Yaya Toure ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka ya barani Afrika usiku wa leo kwenye sherehe zilizofanyika nchini Lagos, Nigeria.

Kiungo huyo sasa ameungana na Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Et'oo kuwa wachezaji wawili kuwahi kushinda tuzo hiyo mara nne huku Yaya Toure, akiwa na upekee kidogo kwani ameshinda mara nne mfululizo tangu alipochukuwa kwa mara ya kwanza mwaka 2011.

Toure awamu hii ameshinda tuzo hiyo mbele ya mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang na Golikipa wa Nigeria, Vincent Enyeama ambao walitinga kwenye hatua ya tatu bora.

Tuzo hiyo ya Yaya Toure imetokana na uwezo uliouonyesha akiwa na klabu ya Manchester City kuliko timu ya taifa. Yaya aliweza kufunga bao kwenye fainali ya Capital One Cup msimu uliopita dhidi ya Sunderland na kufunga mabao 20 kwenye ligi kuu wakati Manchester City wakiibuka mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza.

Yaya hakuwa na mwaka mzuri kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa sababu Ivory Coast walishindwa hata kuvuka kwenye hatua za makundi kwenye fainali za kombe la Dunia nchini Brazil kutokana na bao la dakika za lala salama walilofungwa dhidi ya Ugiriki huku wakichechemea pia katika kufuzu kwa michuano ya AFCON 2015.

Kiungo huyo amewahi kushinda tuzo hiyo mbele ya Seydou Keita (Mali) mwaka  2011, Drogba mwaka 2012 na John Obi Mikel wa Nigeria mwak 2013. Toure ndiye nahodha kwa sasa wa Ivory Coast na atakiongoza kikosi cha nchi yake kwenye fainali za AFCON mapema mwezi huu huko Guinea ya Ikweta.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!