Alexies Sanchez aibeba Arsenal.
Na Oscar Oscar Jr
Likiwa ni goli la 12 kutoka kwa mshambuliaji mahiri wa Arsenal, Alexies Sanchez ambaye alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa leo dhidi ya Stpke City ambao ulimalizika kwa Gunners kushinda mabao 3-0 huku Laurent Conscienly akifunga pia bao moja katika ushindi huo.
Matokeo hayo ni isharatosha kuwa Gunners wanaendelea kujiwekea uhakika wa kumaliza kwenye moja ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.
Arsenal sasa wametinga kwenye nafasi ya tano wakiwa na alama 36 huku timu za Southampton, Manchester United, Manchester City na Vinara wa ligi hiyo Chelsea, zikisalia juu ya vijana wa Kocha Arsene Wenger.
Katika mchezo huo, Arsenal ilishuhudia beki wake Matthieu Debuchy akipata tatizo la kuteguka bega baada ya kugongana na kiungo mshambuliaji wa Stoke City, Marko Arnautovic na kutolewa nje kwa machela.
Mchezo huo pia ulishuhudia kipa namba moja wa timu hiyo, Wojciech Szczesny akiachwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na David Ospina.
Szczesny ambaye alionekana kuwa chini ya kiwango kwenye mchezo uliopita dhidi ya Southampton ambao Gunners walipoteza kwa bao 2-0, hivi karibuni alikamatwa akivuta Sigara na kocha wake aliamua kumpa adhabu na kumpiga faini.
0 comments:
Post a Comment