Azam Fc wameamua kuvunja ukimya.
Baada ya timu hiyo kucheza michezo minne ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao nchini Uganda na kufanikiwa kushinda mchezo mmoja tu huku wakifungwa kwenye michezo mitatu, jambo hilo limeanza kuzua hofu na kuhoji ubora wa timu hiyo kwa baadhi ya wadau.
Azam waliporejea kwenye ligi kuu Tanzania bara, walitoka sare ya bao 2-2 na Yanga na sasa wapo Zanzibar kwenye michuano ya kombe la Kagame huku mchezo wao wa kwanza wakitoka sare ya kufungana bao 2-2 na mabingwa KCCA ya nchini Uganda kwenye mchezo ambao walionekana kuutawala huku wadau wa soka wakiendelea kuhoji uwezo wa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo na benchi lao la ufundi.
Kutokana na hali hiyo, timu hiyo kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Mabingwa wa Zanzibar KMKM, wametoa taarifa ambayo unaweza kutafsiri kama majibu ya minong'ono ya watu juu uwezo wa benchi lao la ufundi na baadhi ya wachezaji.
Taarifa kutoka ukurasa wa Facebook wa Azam Fc inasomeka kama ifuatazo:
Azam FC leo itashuka dimbani kukwaana na KMKM katika mechi za kuwania kutwaa kombe la mapinduzi. Mechi hizi ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya CAF... Makocha wanajaribu wachezaji na mifumo tofauti ambayo wataitumia kwenye mechi za CAF.
Wengi tumehoji sare ya 2-2 na KCCA, naomba tukumbushane tuu kuwa KCCA ni mabingwa watetezi na timu ngumu. Pia Azam iliingia uwanjani bila wachezaji saba wa kikosi cha kwanza. Hebu tuchukulie mfano Chelsea kuingia uwanjani bila ya wafuatao
1. Courtois (Aishi)
3. Azqulipeta (Gardiel)
5. Wawa (Terry)
6. Matic (Bolou)
8. Fabregas (Domayo)
9. Costa (kavumbagu)
11. Hazard (Kipre)
Hatusemi waliocheza si wazuri... Hapana wachezaji wetu wote wazuri lakini kila timu ina uti wa mgongo na hao niliowataja ni wachezaji wa kikosi cha kwanza
Azam ilianza ligi na majeruhi wengi akiwemo Captain Bocco... Tunashukuru Mungu majeruhi wote wamerejea... Wote wapo mazoezini na benchi la ufundi na utabibu wanawaingiza uwanjani kwa mujibu wa ratiba za kitabibu.
Mchezaji pekee mbaye atasubiri wa majuma machache ni Kimwaga
Tulikuwa na majeruhi na wagonjwa wafuatao
Bocco
Domayo
Kimwaga
Brison
Kevin Friday
Tunachotakiwa sasa ni kushikamana kama timu... Kuwa kitu kimoja...
Makocha tulionao ni wa kiwango cha CAF. Kocha wetu mkuu ni mzoefu wa mashindano makubwa na ni mshindi akiwa na medali ya Dhahabu ya CAF Champions League & Confederations Cup kwa kuziongoza Corton Sports ya Cameroon na AC Leopards ya CONGO, Akiwa na Medali ya Fedha ya AFCON na CHAN akiiongoza Cameroon.
Pia akiwa na uzoefu wa kuongoza taifa kubwa la Cameroon Kombe la Dunia mara mbili kama kocha Msaidizi (Ufaransa na Korea-Japan)
Ni kocha huyu huyu ambaye mwaka jana alitupa ubingwa wa Tanzania baada ya kutolewa mechi ya awali na timu ya Msumbiji. Kama tungefanya maamuzi ya Mtani Jembe basi na ubingwa tusingetwaa..
Uongozi unawapa kila aina ya ushirikiano benchi la ufundi na tuna imani nao... Mungu ibariki Azam FC, Mungu Ibariki Tanzania. Mapinduzi ya soka Yanaendelea.
0 comments:
Post a Comment