Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 December 2014
Saturday, December 27, 2014

Khedira bado yupo yupo sana.


Na Chikoti Cico


Kiungo mkabaji wa timu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani, Sami Khedira ambaye amekuwa akihusishwa kusajiliwa na timu mbalimbali zikiwemo Arsenal na Chelsea za Uingereza pia na Bayern Munich ya Ujerumani amesisitiza kwamba bado anapenda kuendelea kuichezea timu ya Madrid.

Wakati dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufunguliwa mapema wiki ijayo huku mkataba wa Khedira ambao unaisha mwakani kwenye majira ya joto hivyo Madrid wanataka kumuuza kiungo huyo kwenye dirisha hilo la usajili kuliko kumpoteza bure.

Mkataba wake utakapoisha wakati huo huo kuanzia Januari mosi timu kutoka nje ya Hispania zinaweza kumsajili mchezaji huyo.

Akiongea na gazeti la Stuttgarter Nachrichten la nchini Ujerumani Khedira alipoulizwa kama anataka kuendelea kubaki Real Madrid alisema “kama tutafikia mwafaka nitakuwa na furaha”

Khedira ambaye muda mrefu amekuwa akihangaika na majeraha toka msimu uliopita ana changamoto kubwa ya kucheza mbele ya Modric na Kroos ambao wamekuwa wakipewa nafasi dhidi yake huku pia Isco na Asier Illaramendi wakionekana kupewa nafasi zaidi kwenye kikosi cha Madrid.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!