Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 December 2014
Wednesday, December 31, 2014

Timu zinazobebwa kwa magoli ya Penati mpaka sasa EPL


Na Chikoti Cico

Baada ya Chelsea kunyimwa penati kwenye mchezo dhidi ya Southampton na mwamuzi Anthony Taylor hatimaye takwimu zimetoka zinazoonyesha nani ni vinara wa kupewa penati na nani hawajui hata magoli ya penati yanafanyaje kwenye timu zao katika ligi kuu nchini Uingereza ambayo inakaribia kuanza mzunguko wa pili kwenye msimu wa mwaka 2014/15.

Timu ya Manchester City ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza ikiwa na alama 43 ndiyo timu inayoongoza kwa magoli ya penati, mpaka sasa wamepewa penati tano toka ligi imeanza huku kiungo Yaya Toure, akiwa mpigaji wao mahiri katika sehemu kubwa ya penati hizo.


Nyuma ya Manchester City wanaofuata kwa magoli ya “matuta” ni “washika bunduki wa jiji la London” timu ya Arsenal ambao mpaka sasa wamepewa penati nne pamoja na West Bromwich Albion huku penati hizo zikiisaidia Arsenal kufikisha alama 33 na kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi katika mechi 19 kwa upande wa West Brom hali ni tofauti kwani mpaka sasa wanashika nafasi ya 16 wakiwa na alama 17.

Queens Park Rangers, Crystal Palace na Everton wanashika nafasi ya tatu katika orodha ya timu zilizopata penati nyingi kwenye mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza huku wote wakipewa penati tatu kila mmoja na waamuzi mbalimbali katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Nafasi ya nne imeshikwa na Chelsea, Burnley, Leicester City, na Stoke City ambao kila mmoja alipata penati mbili katika mechi 19 walizocheza kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo maarufu kama “Barclays Premier League”.

Huku Chelsea amabo karibuni kocha wao amelalamika kwamba kuna “kampeni ya chinichini” ya kuinyima Chelsea penati kutoka kwa marefa, walipata penati zao katika michezo miwili dhidi ya QPR na Arsenal peke yake ambazo zilichezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Pia Southampton, Tottenham Hotspur, Sunderland, Newcastle United, Liverpool, West Ham United, Hull City na Swansea City nao walibahatika kupata penati huku kila timu ikipata penati moja moja katika michezo waliyocheza.


Katika timu ambazo mpaka mzunguko wa kwanza wa ligi kuu nchini Uingereza unafikia tamati hawajawahi kupata penati katika mchezo wowote kati ya michezo 19 ni Manchester United mbayo inafundishwa na kocha Louis van Gaal na Aston Villa

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!