Sanchez ni moto wa kuotea mbali.
Likiwa ni bao lake la 14 kwenye mashindano yote na la tisa kwenye ligi kuu tangu alipojiunga na timu ya Arsenal akitokea klabu ya Barcelona, Alexies Sanchez aliweza kuwapatia alama tatu muhimu vijana hao wa kocha Arsene Wenger ambaye kwa sasa, mashabiki na wapenzi wa timu hiyo wanaonekana kutomwamini tena.
Fraser Forster ni moja kati ya walinda mlango bora kabisa msimu huu huku akiwa anaongoza kwa kukaa langoni mechi nyingi bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa (Clean Sheets).
Jana Golikipa huyo alijikuta kwenye wakati mguu pale Sanchez alipounganisha pasi ya kiungo Aaron Ramsey mnamo dakika ya 89 ya mpambano na kuwapatia Gunners goli pekee la ushindi.
Forster alikuwa imara sana huku mara kadhaa akiokoa mashutu ya Danny Welbeck na baaadaye Oliver Giroud ambaye kwenye mchezo wa jana alianzia benchi. Ushindi huo umewafanya vijana wa Wenger kutimiza alama 23 na kusalia kwenye nafasi ya sita.
Bado hakuna matumaini yoyote kwa vijana wa Gunners kuweza kutwaa ubingwa wa ligi ku ya Uingereza kwani, tofauti yao na vinara Chelsea kwa sasa ni alama 13.
Chelsea baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Spurs wametimiza alama 36 huku ushindi wa Manchester City wa bao 4-1 dhidi ya Sunderland, unawafanya wabaki nafasi ya pili wakiwa na alama 30 na Southampton wanabakia nafasi ya tatu wakiwa na alama 26.
Mashabiki wa Emirates walikuwa wameanza kuingiwa na wasiwasi na hata kuanza kupiga kelele dakika ya 65 pale Wenger alipoamua kumwingiza straika Mfaransa, Giroud kuchukuwa nafasi ya Oxlade-Chamberlain.
Giroud alibadilisha mambo na akamlazimisha Forster kufanya kazi ya ziada kukiwa na dakika chache zilizosalia. Baada ya Giroud kuvuruga mambo eneo la hatari la Southampton, Ramsey alitwaa mpira na akatoa krosi kutoka upande wa kulia iliyomfikia Sanchez ambaye alimpoteza Forster na mpira kutinga wavuni.
0 comments:
Post a Comment