Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Algeria wapangwa kundi la kifo AFCON.



Algeria ndiyo nchi inayoshika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya viwango vya Fifa kwa timu zinazotoka bara la Afrika baada yao kufika 16 bora katika Kombe la Dunia mapema mwaka huu nchini Brazil na kushinda mechi tano kati ya sita walizocheza za kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika katika kipindi cha miezi mitatu.

CAF jana walichezesha droo na kupanga makundi ya michuano ya Afrika ambayo inatarajia kutimua vumbi mapema mwezi January nchini Guinea ya Ikueta huku kundi C, likitajwa na wengi kama kundi la kifo.
 
Algeria wamewekwa pamoja na Ghana na timu hatari za Senegal na Afrika Kusini. Afrika Kusini walimaliza wakiwa vinara wa kundi lao ambalo lilipelekea kushindwa kufuzu kwa mabingwa watetezi, timu ya taifa ya Nigeria. Senegal nao walifanikiwa wakabandua Misri walioshinda kombe hilo mara nyingi zaidi. 
 
Ghana wataenda kwenye michuano hiyo wakiwa na kocha mpya Avram Grant baada ya kupewa kazi hiyo wiki iliyopita. Wenyeji Equatorial Guinea, waliochukua nafasi ya Morocco kuwa wenyeji miezi miwili tu kabla ya mtanange huo wa timu 16 kufanyika kuanzia Januari 17 hadi februari 8, watafungua dimba hilo mjini Bata dhidi ya Congo. 
 
DROO KAMILI
Kundi A - Equatorial Guinea, Congo, Gabon, Burkina Faso
Kundi B - Zambia, DR Congo, Cape Verde, Tunisia
Kundi C - Ghana, Senegal, Afrika Kusini, Algeria
Kundi D - Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!