Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 December 2014
Saturday, December 27, 2014

Gareth Barry na rekodi yake ya uchafuzi.


Na Chikoti Cico

Kiungo mkabaji wa timu ya Everton, Gareth Barry avunja rekodi ya mchezaji aliyeonyeshwa kadi nyingi za njano kwenye historia ya ligi kuu nchini Uingereza baada ya kufikisha kadi 100 za njano kwenye mchezo dhidi ya Stoke City ambapo Everton walifungwa kwa goli 1-0.

Barry alionyeshwa kadi ya njano ya 100 na mwamuzi wa mchezo huo dhidi ya Stoke Lee Mason baada ya kumchezea vibaya Steven Nzonzi huku ikiwa ni kadi ya njano ya sita kwa Barry toka kuanza kwa msimu huu.

Huku akiwa na miaka 33 Barry kwa ujumla amecheza mechi zaidi ya 500 akizichezea timu za Aston Villa, Manchester City na Everton na kutokana na kucheza eneo la kiungo ambapo ni kama injini ya timu kupata kadi ya njano ni jambo ambalo linategemewa mara nyingi akiwa uwanjani.

Lee Bowyer ambaye alizichezea timu za Leeds United, West Ham, Newcastle na Birmingham kwenye nafasi ya kiungo kabla ya kustaafu soka pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Blackburn, Southampton na Bolton Kevin Davis ambaye kwasasa anaichezea timu ya ligi daraja la kwanza ya Preston kwa pamoja wanamkaribia Barry kwa kuonyesha kadi nyingi za njano huku wote wakiwa wameonyeshwa kadi 99.

Kiungo za zamani wa Manchester United Paul Scholes anashika nafasi ya nne akionyeshwa kadi 97 za njano wakati akiichezea United huku Scott Parker akishika nafasi ya tano akionyeshwa kadi 92 za njano wakati akizichezea klabu za Fulham, Charlton na Fulham.

Robbie Savage ambaye aliwahi kuzichezea timu za Birmingham City na Blackburn ambapo ndani ya msimu wa mwaka 2003/2004 akiwa Birmingham alipewa kadi 13 za njano anashika nafasi ya sita huku George Boateng, akishika nafasi ya saba akionyeshwa kadi 85 wakati akizichezea timu za Coventry City, Aston Villa, Middlesbrough na Hull City

Mchezaji wa zamani wa Bolton na Newcastle Kevin Nolan ambaye kwasasa anaichezea timu ya West Ham anashika nafasi ya nane akionyeshwa kadi 83 za njano sawasawa na Wayne Rooney ambaye anashika nafasi ya tisa lakini akiwa naye ameonyeshwa kadi 83 za njano toka akiichezea Everton na sasa Manchester United.

Anayemaliza “top 10” ya wachezaji wenye kadi nyingi za njano ni Philip Neville ambaye alionyeshwa kadi 82 za njano wakati akizichezea timu za Everton na Manchester United.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!