Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 December 2014
Saturday, December 27, 2014

Mastaa wameendelea kupigwa chini.


Na Chikoti Cico
 
Kocha wa timu ya taifa ya Senegal Alain Giresse amtema mshambuliaji wa zamani wa Newcastle na Chelsea Ibrahim Ba ambaye kwasasa anaichezea kabla ya Besiktas ya Uturuki kwenye kikosi cha utangulizi cha wachezaji 28 kuelekea kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini Equatorial Guinea kuanzia Januari 17 mwakani.

Ba ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri akiichezea timu ya Besiktas kwenye ligi ya Uturuki na kwenye michuano ya EUROPA pia aliiwakilisha timu ya taifa ya Senegal kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2012 ambapo timu hiyo ilitolewa kwenye raundi ya kwanza.

Senegal maarufu kama “Simba wa Teranga” wamepangwa kundi C pamoja na Afrika ya Kusini, Ghana na Algeria.
Kikosi cha utangulizi cha Senegal kilichotajwa ni:

MAKIPA: Bouna Coundoul (Ethnikos Achnas FC/CYP), Lys Gomis (Trappani/ITA), Pape Demba Camara (Sochaux/FRA), Ousmane Mane (Diambars) MABEKI: Zargo Toure (Le Havre/FRA), Lamine Gassama (Lorient/FRA)

Wengine ni Lamine Sane (Bordeaux/FRA), Kara Mbodj (Genk/BEL), Pape Ndiaye Souare (Lille/FRA), Papy Djilobodji (Nantes/FRA), Boukary Drame (Atalanta/ITA), Ibrahima Mbaye (Inter Milan/ITA), Cheikh Mbengue (Rennes/FRA)

VIUNGO: Cheikhou Kouyate (West Ham Utd/ENG), Pape Kouli Diop (Levante/ESP), Idrissa Gana Gueye (Lille/FRA), Stephane Badji (Brann/Nor), Salif Sane (Hanover/GER), Pape Alioune Ndiaye (Bodo Glimt/NOR), Alfred Ndiaye (Real Betis/ESP).

WASHAMBULIAJI: Moussa Konate (SC Sion/SUI), Diafra Sakho (West Ham Utd/ENG), Mame Birame Diouf (Stoke City/ENG), Sadio Mane (Southampton/ENG), Moussa Sow (Fenerbahce/TUR), Papiss Demba Cisse (Newcastle Utd/ENG), Henri Saivet (Bordeaux/FRA), Dame Ndoye (Lokomotiv Moscow/RUS).

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!