Donald Mosoti kurejea Simba.
Na Oscar Oscar Jr
Beki wa kimataifa wa Kenya, Donald Mosoti anatajwa kurejea tena kwenye klabu ya Simba ambapo beki huyo aliachwa wakati wa usajili kuelekea msimu huu kutokana na idadi ya wachezaji wa kigeni kuzidi watano hivyo Simba, wakamtoa sadaka.
Mosoti mwenyewe amekaririwa akisema kuwa hana tatizo lolote kurudi tena kuitumikia klabu ya Simba lakini ni lazima wakae tena mezani na Uongozi wa Simba ili kujadili upya masharti ya mkataba wake.
Musoti alijiunga na Simba wakati wa dirisha dogo msimu uliopita na kuonyesha kiwango bora kabisa lakini ulipoingia Uongozi mpya wa Simba, haukuona sababu za kuendelea na beki huyo.
Simba kwa sasa inaonekana kuyumba kwenye eneo la Ulinzi na hali hiyo imethibitika kwenye michezo mitano ya ligi kuu Tanzania bara ambapo Simba walikuwa wanatangulia kupata goli lakini, baadaye, mabeki wa timu hiyo wanaoongozwa na Joseph Owino, walishindwa kuhimili vishindo vya wapinzani wao.
Abdi Banda na Joramu Mgeveke ndiyo walinzi ambao hawajapa nafasi kwenye kikosi cha kocha Mzambia, Patrick Phiri ambaye kila kukicha, anakuja na orodha tofauti ya wachezaji wanaoanza kwenye kikosi cha kwanza.
Mosoti kwa sasa yuko na Tusker Fc ya nchini Kenya na tayari Uongozi wa timu hiyo umesema hauna kikwazo kama mchezaji huyo ataamua kurudi Simba kwani, Mosoti aliwaomba tu acheze kwenye timu yao ili kulinda kipaji chake.
0 comments:
Post a Comment