Na Oscar Oscar Jr
Ikiwa ksho ndiyo dirisha la usajili linafunguliwa Tanzania bara, klabu nyingi zinaonekana kuwa kwenye harakati za kuingiza na kutoa wachezaji kwenye klabu zao lakini, habari ni tofauti kwa Mtibwa Sugar ambao ndiyo vinara wa ligi kuu.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Mexime amebainisha kuwa haoni sababu ya kusajili wachezaji wengine wakati hawa alionao kwa sasa wanatimiza majukumu yao uwanjani kama kawaida.
Mtibwa Sugar ambayo iliwahi kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara mbili mfululizo, imejipanga kuhakikisha kuwa msimu hu wanarejea kile walichokifanya mwaka 1999 na 2000.
Timu hiyo tayari imekutana na timu za Yanga, Simba na Mbeya City na kuvuna pointi saba kati ya tisa. Hii ni ishara nzuri kwao kwani hizo ni moja kati ya timu zinazopigiwa upatu wa kuweza kutwaa ubingwa msimu.
Mtibwa ndiyo timu yenye safu bora ya ushambuliaji kwenye ligi kuu wakiwa tayari wamefunga mabao 10 huku mshambuliaji Ame Ally akiwa na mabao manne, Ally Shomary akiwa na mabao matatu na Mussa Hassani "Mgosi" akiwa na mabao mawili.
Mzunguko wa nane wa ligi kuu, utaanza tarehe 26 Desemba huku Mtibwa wao wakiwa nyumbni watawakaribisha Stand United kutoka mkoa wa Shinyanga kwenye dimba la Manungu- Morogoro. Stand kwa sasa wanashika nafasi ya 10 kwenye msimamo na watataka kupata pointi tatu ugenini ili kujiweka sawa kwenye nafasi nzuri itakayowahakikishia kubaki ligi kuu.
Matokeo ya mtibwa msimu huu
Mtibwa Sugar 2-0 Yanga
Mtibwa Sugar 3-0 Ndanda Fc
Mtibwa Sugar 1-0 Mgambo Jkt
Polis Moro 0-0 Mtibwa Sugar
Mbeya City 0-2 Mtibwa Sugar
Mtibwa Sugar 1-1 Simba Sc
Mtibwa Sugar 1-1 Kagera Sugar
0 comments:
Post a Comment