Yanga majina makubwa ya Bure
Na Oscar Oscar Jr
Yanga ni moja kati ya timu ambazo kabla ya msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara kuanza kutimua vumbi, ilikuwa inapewa nafasi kubwa sana ya kushinda taji la ligi kuu huku watu wakitarajia kuona soka maridadi kutokana na usajili waliofanya.
Bado ya Yanga wananafasi ya kutwaa Ubingwa huo kwani ushindi wao wa mechi yao dhidi ya Mgambo JKT kwenye dimba la Taifa Jumamosi ya wiki iliyopita, umewafanya wasogee hadi kwenye nafasi ya pili huku wakiwa na pointi 13 na kuzidiwa alama mbili pekee na vinara wa ligi hiyo, Mtibwa Sugar ambao walitoka sare ya 1-1 na timu ya Kagera Sugar na kufikisha alama 15.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwanaspoti la leo, kipa wa Mgambo JKT amewaponda wachezaji wa Yanga kutokana na kuwa na majina makubwa kuliko uwezo wao Uwanjani.
Akiongea na Gazeti hilo, Said Lubawa alimpongeza kipa wa Yanga, Dida na kuwaponda wachezaji kama kiungo mshambuliaji, Mrisho Ngassa na kusema kuwa, mchezaji huyo kiwango kimeshuka.
Mrisho Ngassa ambaye aliibuka mfungaji bora wa Yanga msimu uliopita baada ya kufunga magoli 13, msimu huu haujawa mzuri sana kwake na pengine sio yeye pekee.
Wachezaji wengi wa timu hiyo bado hawajacheza kwa kiwango ambacho watu wengi walitarajia hali inayofanya watu kuhoji mbinu za kocha Maximo kama zinahusika katika hili.
Mpaka sasa, mshambuliaji Simon Msuva ndiyo anaonekana kuwa kwenye kiwango cha juu kabisa na mabao yake mawili iliyofunga akitokea benchi kwenye mchezo wao na Mgambo, yanathibitisha ubora wake.
Msuva amefunga magoli matatu mpaka sasa huku, Jerryson Tegete akimfuatia kwa kufunga mabao mawili. Mpaka sasa, Yanga imefunga mabao tisa na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara tano.
Picha hiyo ni kwa hisani ya Global Publishers
0 comments:
Post a Comment