Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 November 2014
Tuesday, November 11, 2014

Wayne Rooney awaiga Booby Moore na Steven Gerrard.


Na Chikoti Cico

Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney anatarajia kufikisha michezo 100 ya kuichezea timu ya taifa ya England maarufu kama “Three Lions” kwenye mchezo dhidi ya Slovenia katika mechi za kufuzu michuano ya Euro 2016 huku akitarajia pia kukabidhiwa kofia ya dhahabu kama ishara ya utambulisho kwa mchango wake kwa timu ya taifa.

Rooney ambaye anaungana na Peter Shilton, David Beckham, Steven Gerrard, Bobby Moore, Ashley Cole, Frank Lampard, Bobby Charlton na Billy Wright katika kufikisha michezo 100 ya timu ya taifa ya Uingereza.

Rooney alirejea kwenye shule ya msingi aliyosoma zamani kitendo kilichowahi kufanywa na Booby Moore na Steven Gerrard walipofikisha michezo 100 wakiichezea Three Lions ikiwa kama ishara ya kufurahia kufikisha michezo hiyo.

Rooney alirejea kwenye shule ya Our Lady and St Swithin’s Catholic Primary School iliyoko jijini Liverpool na kupata wasaa wa kupiga picha na wanafunzi 99 na pia kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na kusaini jezi za timu ya taifa ya Uingereza zilizovaliwa na wanafunzi hao kama zawad, Kitendo kilichowafurahisha mno wanafunzi wa shule ya Our Lady and St Swithin’s Catholic Primary School.

Rooney akiongea baada ya tukio hilo la kipekee shuleni hapo alisema “ Ulikuwa wakati maalum kurejea kwenye shule ambayo nilienda kama kijana mdogo, niliona walimu wachache wa zamani ambao walikuwa hapa wakati nasoma na ilikuwa vizuri kuwaona watoto wakifurahi. Hapa ndipo nlipoanza kuupiga mpira”.

Aliendelea kusema “Watoto wote hapa wana ndoto. Vijana wote wanakua wakitaka kuwa wachezaji mpira, wanaupenda mchezo wa soka.

Nilikuwa hivyo nilipokuwa hapa nilitaka kuwa mchezaji mpira wa kulipwa na nimeweza kufanya hivyo. Kwahiyo kuwa nahodha wa nchi yangu na kukaribia michezo 100 ni maalum na ni vizuri kwa shule pia. Ninajivunia nilipotokea na ni vizuri kwamba naweza kurejea kwenye eneo hili”

Rooney aliendelea kusema “ Wote wanajua naichezea Manchester united na natumaini wanajivunia kwa ambacho nimekifanya kwenye kazi yangu, natumai inawahamasisha, kwa watoto kumwona mtu ambaye alikuwepo kwenye shule hii na alienda kufanikiwa kwa nilichokifanya kinaonyesha wanaweza kufanikiwa ndoto zao”

“Najua inavyokuwa, Franny Jeffers alienda kwenye shule yangu ya Sekondari (De La Salle) na alinihamasisha mimi. Itakuwa vizuri kufikiri kwamba itakuwa vivyo hivyo kwa hawa”.

Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo Sandra Hamilton akimwongelea Rooney alisema “ Wayne anawapa watoto kujiamini na ana kila thamani tunayoithamini, amekuwa mtu mzima mwenye mafanikio, kiongozi. Ni mtu wa daraja la juu duniani tunamwangalia kama mwanaume bora wa familia na tunajivunia sana kwa kila kitu anachokifanya.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!