Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 November 2014
Tuesday, November 11, 2014

Christiano Ronaldo apokea tuzo na kumkumbuka Alfredo di Stefano.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ta Ureno, Christiano Ronaldo amkumbuka mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Alfredo Di Stefano wakati wa upokeaji tuzo ya mfungaji bora wa la liga kwa msimu uliopita na mchezaji bora wa mwaka hivyo alipewa tuzo ya pichichi na tuzo ya Di Stefano.

Mshambuliaji huyo (Di Stefano) kutoka Argentina ambaye aliisaidia Madrid kushinda kombe la Ulaya mara tano mfululizo kuanzia 1956-60 na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 1957 na 1959 huku pia akipewa kuwa raisi wa heshima wa Madrid alifariki mwezi wa saba mwaka huu kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo akiwa na miaka 88.

Ronaldo akiongea baada ya kupokea tuzo hiyo alisema “ Nataka kuchukua nafasi hii kusema kwamba ni vibaya kwamba Don Alfredo Di Stefano hawezi kuwa hapa kunipa tuzo.

Ronaldo ambaye amekuwa akifananishwa na Di Stefano pia aliongeza kwa kusema “ Nimeangalia video nyingi za kwake kwasababu sikumwona akiwa anacheza na alikuwa bora, kuhusishwa nae ni nafasi ya peke na heshima.

Ni kitu ambacho kinanipa hamasa ya kufanya kazi zaidi. Nilimjua kwa ukaribu tangu nilipofika Madrid na kwangu alikuwa mtu wa tofauti.

Ronaldo ambaye aliongoza kwa ufungaji wa magoli msimu uliopita la liga kwa kufunga magoli 31, toka kuanza kwa msimu huu ameshafunga magoli 23 kati ya mechi 17 alizoichezea Madrid huku magoli 18 akiyafunga kwenye ligi na kuisaidia Madrid kuongoza msimamo wa la liga wakiwa juu ya Barcelona kwa alama mbili zaidi baada ya michezo 11.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!