Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 November 2014
Sunday, November 16, 2014

Wachezaji wa kigeni hati hati Msimbazi.


Na Oscar Oscar Jr

Wachezaji wa kigeni wa Simba kwa sasa, wanatakiwa kukaa mguu mmoja nje na mwingine ndani kwani muda wowote wanaweza kufungashiwa virago. 

Baada ya dirisha la usajili kufunguliwa hapo jana, Simba wameripotiwa kuwanyatia wachezaji wawili wa kutoka nje ya nchi huku Donald Mosoti akitajwa kurejea tena msimbazi.

Mshambuliaji wa klabu ya APR ya Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza na Danny Sserunkuma raia wa Uganda ambaye anakipa na mabingwa wa Kenya, timu ya Gor Mahia wametajwa kutua Msimbazi kwenye dirisha hili la usajili ambalo litafungwa Desemba 15.

Simba tayari inawachezaji watano wa kigeni na ili wachezaji hao waweze kusajiliwa ni lazima wachezaji wengine watoke. Pierre Kwizera na Amisi Tambwe ni wachezaji ambao muda wowote wanaweza kuonyeshwa mlango wa kutokea kutokana na kushindwa kutamba msimu huu.

Klabu ya Simba imeendelea pia kuhusishwa na kumrejesha kikosini beki wa kati kutoka nchini Kenya, Donald Mosoti ambaye aliomba kujiunga na timu ya Tusker ya nchini Kenya ili kulinda kipaji chake baada ya kuachwa na Simba bila kuwepo kwa sababu za msingi msimu huu.

Simba inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ingawa haijapoteza mchezo wowote baada ya kushuka dimbani mara saba huku wakitoka sare mara sita na kupata ushindi mara moja.

Wekundu hao wa Msimbazi watalazimika kumuacha tena mchezaji mwingine kama kweli wanataka kumrejesha Mosoti. Mpaka sasa wachezaji wa kigeni wenye uhakika wa kubaki na mabingwa hao mara 18 wa ligi kuu Tanzania bara ni Emmanuel Okwi na Joseph Owino tu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!