Searching...
Image and video hosting by TinyPic
14 October 2014
Tuesday, October 14, 2014

Uchambuzi Yanga vs Simba Octoba 18



 Na Samuel Samuel

Wakati Simba inaingia uwanjani huku wadau wengi wa soka wakiipa nafasi yanga kushinda kutokana na fowadi line yake na kuyumba kwa backline ya Simba, lakini Yanga imegumbikwa na jinamizi la kihistoria. Mara zote Simba inapokuwa dhaifu katika ligi imekuwa ikipata matokeo ya kushangaza dhidi ya Yanga. 

Hebu tuvitazame vilabu vyote viwili. Simba inaundwa na wachezaji vijana na wenye nia ya kuudhirishia umma kuwa wanataka kuendeleza vizuri historia ya Simba na kujenga jina kwa vipaji walivyonavyo. 

William Lucian full back right, ana uwezo mzuri wa kupandisha timu na kusaidia mashambulizi, Kama Maximo atampanga Jaja huyu ana uwezo mzuri kumpa back up Owino au Hassan Isiaka ili Niyonzima , Twite au winga za Yanga zisimpe mipira ya mwisho. 

Phiri ana uwezo mkubwa wa kutengeneza mfumo wa kutumia viungo wengi ili kuizuia Yanga isitawale pale kati. Ana wachezaji mahiri kama Said Ndemla, Kwizera, Mkude, Amri Kiemba na Uhuru Selemani. Anaweza akatumia 4-3-1-2 . 

Winga ya kulia akicheza Said Ndemla, kushoto, Okwi na kiungo mkabaji akasimama Kwizera. Fomesheni hiyo itamuacha Amri Kiemba acheze kama free mid fielder ili wapambane vizuri na Haruna Niyonzima . Itakuwa ni mechi nzuri sana. 

Upande wa kushoto kuna baba ubaya ndio upande imara kwenye ngome ya Simba. Ubaya ana uwezo mzuri wa kuituliza fowadi line ya timu pinzani kutokana na kutokuwa na papara anapokaba. 

Kingine huyu akipewa nafasi atamsadia sana aidha Okwi au Singano upande wa kushoto kutokana na uwezo mkubwa wa kupandisha timu na kurudi kukaba. 

Tatizo lipo kwa golikipa Casilas bado hajaonesha ukomavu wa kuhimili mikiki mikiki ndani ya Simba. Anashindwa kuipanga back line yake vizuri. 

Pia sare zinazoendelea zinamtoa katika hali ya kujiamini. Kocha wa makipa anahitajika kumjenga sana kisaikolojia kabla ya mtanange huo. 


Maximo ni mechi yake ya kwanza dhidi ya mahasimu hawa wawili nchini. Lakini si mgeni sana maana akiwa national team alikuwa akiona pressure ilivyo katika kuliandaa pambano la watani wa jadi na nini kilikuwa kikiwakuta wachezaji na makocha baada ya mechi. 

 Maximo kama anahitaji ushindi kwenye mechi hii, kwanza kuwaandaa vizuri wachezaji kisaikolojia. Bado yanga hawana hali ya kujiamini mbele ya Simba kutokana na matokeo ya msimu uliopita na jinamizi baya la kufungwa 5-0 . 

Kwanza kabisa ni lazima akubali mfumo wa 4-5-1 ndio utakao mbeba kama ilivyokuwa katika mechi ya ngao ya hisani dhidi ya Azam. Pili akubali Jaja atokee benchi akimpa nafasi Javu kuanza. Jaja ni mzito kucheza dhidi Uhuru Selemani, Kwizera, Kiemba, Singano au mkongwe Kisiga. 

Maximo anahitaji play maker mwenye kasi na maamuzi ya haraka mwanzo wa mechi . Amruhusu Msuva acheze kama winga wa kulia na kule kushoto ampange Nizar Khalfan. Viungo hao wote ni wazuri kutengeneza nafasi au hata kufunga . 

Kizuri kwao wana uwezo wa kupambana kuliko kumwanzisha Saidi Makapu au Coutinho ambao bado kasi yao ya kutafuta mpira kwenye ushindani ni ndogo. 

Kiungo mshambuliaji Ngasa anafaa kuanza mechi hii lakini atakuwa bora akipunguza chenga zisizo na maana na kufikiria kufunga au kutoa pasi za goli.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!