Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 October 2014
Thursday, October 30, 2014

Samuel Eto'o ni zawadi toka kwa "Mungu wa soka"


Na Oscar Oscar Jr

Kocha wa Everton, Roberto Martinez imeibuka na kusema kuwa mshambuliaji wake ambaye ni raia wa Cameroon, Samuel Eto'o ni kama zawadi kutoka kwa "Mungu wa soka". 

Kocha huyo ameonekana kupagawa na uwezo anaoonyesha mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kucheza kwenye klabu za Real Madrid, Barcelona, Inte Millan na Chelsea.

Eto'o weekend hii, alikuwa kwenye ubora wa hali ya juu na kufunga magoli mawili pale Everton walipoiadhibu timu ya Burnely kwa magoli 3-1 huku mshambuliaji huyo akifunga mara mbili. 

Eto'o msimu uliopita alikuwa na timu ya Chelsea na kati ya washambuliaji watatu wa kocha Jose Mourinho, yeye ndiyo alifunga mabao mengi (12)  kuliko Demba Ba na Fernando Torres.

Martinez ameeleza kuwa, Samuel ni mtu anayejituma kuanzia mazoezini hadi kwenye mechi. Ni mtu pia ambaye uwepo wake, unatoa hamasa kwa vijana ambao wanandoto za kufika mbali kisoka. 

Martinez hakusita pia kumwagia sifa Nahodha wa timu hiyo, Phil Jagielka na kusema kuwa, beki huyo ameongezeka ubora mara dufu tangu kumalizika kwa michuano ya kombe la Dunia.

Everton wanashika nafasi ya tisa wakiwa na pointi 12 baada ya kushuka dimbani mara tisa, huku mshambuliaji Romelu Lukaku na Kelvin Naismith wakiwa na magoli manne kila mmoja na Samuel Eto'o akifikisha magoli matatu ya EPL. 

Weekend hii watakutana na timu ya Swansea City ambao wako kwenye nafasi ya sita.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!