Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 October 2014
Monday, October 13, 2014

Nemanja Matic anapogeuka “mbeba maji”



Na Chicoti jr (Cico cicod) 
0755 7000 76

Chelsea Mwaka 1996 kabla ya mechi ya kombe la mabingwa wa Ulaya (Uefa Champions League) kati ya Manchester United dhidi ya Juventus mchezaji mahiri wa Manchester wakati huo Mfaransa Erick Cantona alipokuwa anahojiwa na waandishi wa habari kabla ya mechi alimzungumzia mchezaji mwenzake kutoka Ufaransa.

 Didie Deschamps alisema “Deschamps wakati wote hucheza kwa asilimia mia moja ila hawezi kuwa chochote zaidi ya mbeba maji tu, na wachezaji kama yeye unaweza kuwapata popote kwenye kona za mtaa” 

Cantona alimaanisha Deschamps ambaye sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa kazi yake kubwa iilikuwa ni kuutafuta mpira na kuwapa wachezaji wengine wauchezee kama Zinedine Zidane na Youri Djorkaeff na kama wakiupoteza tena mpira bado Deschamps atakaba na kuhangaika kuutafuta kuerejesha kwa Zidane na Djorkaeff. 

Didie Deschamps hakupewa miguu ya chenga wala upigaji bora wa pasi wa ZidaneZidane ila alikuwa mpiganaji uwanjani kuhakikisha timu inashinda huku sehemu kubwa ya kazi yake kama kiungo mkabaji ikiwa ni kukaba na kuzuia mashambulizi ya timu pinzani kwa sehemu kubwa ya katikati ya uwanja na hicho ndicho kilichosababisha aitwe “mbeba maji” na Cantona. 

Tukirejea kwenye ligi kuu ya Uingereza kwasasa inawezekana Nemanja Matic ndiye “mbeba maji wa timu ya Chelsea” , mpaka sasa Chelsea inaongoza ligi kuu ya Uingereza huku ikiwa imecheza michezo saba na kushinda michezo sita na kutoka sare mchezo mmoja dhidi ya Manchester City.

kwa mashabiki, wachambuzi wa soka na makocha mbalimbali sifa nyingi zinaelekezwa kwa Fabregas, Hazard na Costa huku Matic akisahaulika kabisa kwa kazi anayoifanya. 

Matic aliyesajiliwa na Chelsea kwa mara ya kwanza mwaka 2009 kutoka MFK Košice na miaka miwili baadaye Matic alihamia timu ya Benfica ambako alianza kucheza kama kiungo mkabaji na hatimaye mwaka 2014 kocha Jose Mourinho aliamua kumsajili kwa mara ya pili kuja kuichezea Chelsea. 

Dili la kumuuza na kumnunua Matic kwa mara ya pili kutoka Benfica inaweza kuonekana kama biashara ya ajabu ila Chelsea ilimhitaji mchezaji wa aina ya Matic ili kuleta uwiano (balance) kwenye timu. 

Chelsea yenye wachezaji kama Fabregas, Hazard, Willian na Oscar kama viungo washambuliaji Matic kama kiungo wa ulinzi analeta uwiano kati ya kushambulia na kukaba, hivyo mpaka sasa Matic anafanya kazi ya kuifanya beki ya Chelsea iwe salama lakini pia kuwezesha kazi ya Fabregas katika kupiga pasi ifanikiwe. 

Matic ni aina ya wachezaji ambao hutegemei kuona ufundi wa chenga na ni ngumu kukupa magoli 20 kwenye msimu ila ukitaka Fabregas apige pasi za mwisho, Hazard kuzisumbua timu pinzani na Costa kufunga basi utamhitaji Matic ili kuleta uwiano huo, namini mpaka msimu huu wa ligi uishe basi Matic “atabeba sana maji” akiwa Chelsea. 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!