Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 October 2014
Sunday, October 26, 2014

Alexies Sanchez shujaa wa The Gunners.


Na Rossa Kabwine

Sunderland yashindwa kuwazuia Arsenal huku kiungo mshambuliaji, Alexis Sanchez akipachika mabao mawili na kuwaacha vijana wa Gus Poyet wakiwa hawala lakufanya.

Goli la kwanza, lilitokana na makosa ya mlinxi wa kati wa Sunderland Wes Brown, akijaribu kumrudishia mpira golikipa wake, Alexies Sanchez aliuwahi na kuwapatia Gunners uongozi wa mchezo.

Bado mambo hayakuwa shwari kwa Sunderland baada ya wiki iliyopita kujikuta wakichapwa magoli 8-0 na Southampton ambayo imeonekana kuwa moto wa kuotea mbali.


Golikipa wa Sunderland Vito Mannone alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kufanya maamuzi sahihi na kujikuta akisababisha goli la pili ambalo lilifungwa pia Sanchez.

Arsenal walijikuta wakipata ushindi wao wa mara nne mfululizo dhidi ya timu ya sunderland katika ligi kuu ya uingereza, lakini arsenal hawakuwa na ushawishi katika mechi hiyo licha ya kuwa waliondoka na pointi tatu.

Arsenal wakicheza katika kiwango kile kile kama walichicheza dhidi ya anderlechet ambapo walifunga goli la ushindi dakika za mwisho wa mchezo katika michuanoa ya klabu bingwa barani ulaya.

Nafasi zilikuwa chache lakiani makosa ya walinzi wa sunderland yaliwapatia arsenal ushindi, bila ya hayo makosa arsenal walipata tabu sana katika kutengeneza magoli Meneja wa sunderland Gus Poyet alisema “ nilitaka kuona wachezaji wawe jasiri wapige pasi na nadahani walikaribia” 

Poyet aliongeza “ hatukufanya makosa katika michezo saba ya kwanza lakini kwa michezo miwili ya mwisho, tumefanya makosa mengi kuliko nilivyotegemea msimu mzima.

Kwa upande wa Arsenal, kocha Arsene wenger alisema “ Tulikuwa tuna miliki mipira lakini sunderland waliweka lengo la kuzuia . walikuja na lengo hilo zaidi kipindi cha pili lakini sisi tulikuwa na nafasi nyingi” 

 Aliongeza pia kuwa katika maisha unaweza kuendelea vizuri lakini muhimu kwetu leo ni kupata pointi tatu na kutoruhusu goli. Magoli hayo mawili ya jana, yamemfanya Sanchez afikishe magoli matano ya EPL.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!